FOMU UHURU MARATHON ZAANZA KUUZWA
Posted in
No comments
Thursday, October 31, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Pichani
kulia ni Innocent Melleck Mratibu Uhuru marathon,akizungumza na
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,mapema jana ndani ya Idara ya HABARI
MAELEZO,kuhusiana na kutangaza rasmi utoaji fomu za usajili kwa ajili
ya mbio hizo jijini Dar es Salaam, ambapo vituo zaidi ya 13
vilifunguliwa katika maeneo mbalimbali.
Innocent
Melleck aliongeza kuwa pia siku ya Jumanne na Jumatano wiki ijayo,
fomu hizo zitatolewa rasmi katika Viwanja vya Bunge, Dodoma ambapo
Mheshimiwa Spika Anne Makinda ndiye anayetarajiwa kuongoza katika
kujisajili, pia katika usajaili huo amewaomba waheshimiwa wabunge
wajiandae na wajitokeze kwa wingi ili kulifanikisha zoezi hilo kwa
ufanisi mkubwa.
Melleck akizungumza mbele ya Wanahabari
Melleck
akionesha fomu za usajili kwa ajili ya shindano hilo,mbele ya
wanahabari (hawapo pichani),aidha ameongeza kuwa anayetaka kushiriki
anaweza pia kujisali kwa njia ya mitandao ya kijamii kama jiachie Blog issamichuzi.blogspot.com www.uhurumarathon.com,mtaa kwa mtaa Blog, mrokit.blogspot.com,kajunason.Blog,weyunga.blogspot.com na blog nyingine
nyiingi.
Katika
usajili huo, fomu zitakazotolewa zitauzwa kwa bei ifuatayo; kwa
mshiriki wa kilomita 3 atalipia Sh 100,000 yule wa kilomita 5 Sh 2,000
na washiriki wa kilomita 21 na 42 watalipia Sh 6,000.
"Kama ambavyo
tumezungumza awali kuwa kesho zoezi hili linaanza rasmi kwa fomu kuanza kuuzwa
na leo hii nawajulisha Watanzania wenzangu kuwa fomu namba moja ya mbio za Km3
itakuwa maalumu kwa Rais Dr.Jakaya Kikwete,ambaye amekuwa
mstari wa mbele kuwahamasisha watanzania kutambua kwa vitendo umuhimu wa kuenzi
umoja,mshikamano na amani iliyopo pasipo kujali itakadi zozote zile,
Pia spika wa
bunge letu tukufu Anna makinda yeye atachukua fomu namba mbili ,fomu namba
tatu itapelekwa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA na mkuu wa
kambi rasmi ya upinzania bungeni na fomu nyingine hadi fomu namba 100 zitakuwa
maalumu kwa ajili ya viongozi wetu mbalimbali wa vyama vya kisiasa, viongozi wa
dini zote na viongozi wa serikali na mashirika binasi",alisema Melleck.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :