MIILI 87 YA WAHAMIAJI YAOKOTWA JANGWA LA SAHARA
Posted in
No comments
Thursday, October 31, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Kulingana na Bwana Alhacen, moja ya magari ambayo wahamiaji hao walikuwa wanatumia kwa usafiri, liliharibika walipotoka mji wa Arlit mwishoni mwa mwezi Septemba, au mwanzoni mwa Oktoba.Maafisa wa usalama pia wamesema kuwa gari la pili liliharibika lilipokuwa njiani kurejea Arlit ili kutengenezwa.
Inaonekana kuwa miongomi mwa wasafiri hao takriban watu 10 walisafari kurejea Arlit na kutoa taarifa ya wenzao kukwama jangwani.Iliarifiwa kuwa miili mitano ilipatikana.Mnamo siku ya Jumatano, wafanyakazi wa kujitolea pamoja na wanajeshi, walipokuwa wanawatafuta wahamiaji hao, wakafanikiwa kupata maiti zaidi umbali wa kilomita 10 kutoka katika mpaka wa Algeria.
Kati ya maiti 48 waliopatikana, kulikuwa na miiili ya watoto na vijana na Alhacen alisema kuwa walikuwa wanaelekea nchini Algeria kutafuta vibarua vya mishahara midogo sana.Akizungumza kutoka katika kiwanda cha kuchimba madini ya Uranium, Kaskazini mwa Agadez, aliambia BBC kuwa hiyo ndiyo iliuwa siku mbaya kwake baada maishani mwake baada ya kupata miili hiyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :