MWANAMKE MTANZANIA ANASWA NCHINI KENYA KWA KOSA LA KUWACHUKUA WALEMAVU TANZANIA NA KUWAFANYISHA BIASHARA MOMBASA KENYA
                      Posted in 
                      
                            No comments
                          
Thursday, October 31, 2013
                      By 
                      danielmjema.blogspot.com
Citizen
 TV ya nchini Kenya wanaripoti kwamba huko Mombasa wamekamatwa watu 26 wenye 
ulemavu ambao walichukuliwa kutoka Tanzania na Mwanamke Mtanzania ili 
kwenda kufanya biashara ya kuomba pesa na baadae jioni Mwanamke huyo 
anapitia mahesabu huku akiwa amewaweka walemavu hawa kuishi kwenye 
nyumba moja huko Mwembe tayari.
Mwanamke huyu anadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza Walemavu kuchukuliwa Tanzania na kuingizwa Kenya kupitia Taveta na Lungalunga ambapo anawatumia kibiashara yeye na washirika wake ambapo mpaka sasa washukiwa saba wametiwa mbaroni kutokana na hii ishu.
Taarifa inasema ombaomba hawa ambao wanatoka Shinyanga, Mwanza, Musoma na Bukoba wakiwa mitaani kuomba, wakipata shilingi mia tano ya Kenya tajiri anachukua shilingi 300 na anamuachia shilingi 200.
Mmoja wa Walemavu hao anasema ‘kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa Baiskeli lakini kinachotokea sasa hivi ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, Mwanamke huyu ndio anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya’
Tazama hapo chini walemavu hao katika video ya Televisheni hiyo wakisimulia masaibu yao na jinsi walivyorubuniwa kuingia nchini Kenya
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
 
 
 
 

 
 
0 MAOINI :