MWIDAU ATAKA KASI YA MAENDELEO JIJINI TANGA

Posted in
No comments
Thursday, October 31, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Mbunge Amina Mwidau akisaini kitabu cha wageni alipotembelea katika ofisi za Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga, kulia ni Mratibu wa chama hicho Neema Hatibu.
Mbunge Mwidau, akipata ufafanuzi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga, Hassan Hashimu.



Mbunge Mwidau akiwa na Ofisa Utamaduni na Michezo wa Wilaya ya Pangani, Kemmy Anatory mara baada ya kuzindua mashindano ya Mwidau CUP.

Mbunge Amina Mwidau, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa Timu ya soka ya wanawake ya Spin Sister, Habiba Hamisi. Timu hiyo ipo Marizala Pongwe jijini Tanga.

Mbunge Amina Mwidau, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa Timu ya soka ya wanawake ya Spin Sister, Habiba Hamisi. Timu hiyo ipo Marizala Pongwe jijini Tanga.

Na Mwandishi Wetu, Tanga

MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), (pichani) amewataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kubadilika kwa kuwa na ari ya kujiletea maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa mjini hapa alipokuwa akizungumza na vionozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga (Tanga Press Club).Alisema kuwa ili maendeleo ya haraka yaweze kupatikana katika mkoa huo ni lazima jamii kubadili kwa kuwa na mawazo chanya.

“Maendeleo ni jambo muhimu sana na katika hili ni lazima tushirikiane kwa dhati. Binafsi ninapenda kupongeza juhudi za chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Tanga kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya katika kutangaza mkoa wetu.

“Nilikuwa nasoma na sasa kila wakati tutakuwa pamoja na wanahabari pamoja na wananchi wa mkoa wetu ili kuweza kuungana kwa pamoja katika juhudi za maendeleo za mkoa,” alisema Mwidau

Mwisho

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .