KASSIM MAPILI KUONGOZA WAKONGWE WENZAKE KATIKA TAMASHA LA GURUMO DESEMBA 14 MWAKA HUU.
Posted in
No comments
Friday, November 29, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Tamasha hilo ambalo ni mahsusi kwaajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe
Muhidini Maalim Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja
vya TCC Club Chang’ombe.Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu
la kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga
Gurumo utakaosikika kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.
Baadhi ya wakongwe wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha la Gurumo
53 ni pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri
Ali.
Gurumo anaagwa kufuatia kutangaza kwake kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.
Bendi za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi
kung’ara na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo
linalosubiriwa kwa hamu.
Hadi kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro
Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni
kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.Wasanii waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza
Gurumo ni pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe,
Mashaka Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni
Ali Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton, na Ibrahim
Mwinchande.
Hata hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo
kwenye tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae”
haitashirki katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Mbizo amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote
litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi
(Disemba 25, 2013).Juma Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini
nyimbo zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo,
zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.
“Wanamuziki wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo,
hawako tena katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji
huyo mkongwe na kushusha burudani nzito.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :