Posted in
By
danielmjema.blogspot.com
|
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ukipita jana, Nov
18, 2013, katika 'mkeka' wa barabara, ulipokuwa ukitoka Namtumbo kwenda
Songea, Kinana akiwa katika ziara mkoani Ruvuma, kukagua utelekezaji wa
ilani ya uchaguzi ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kushirikiana
nao kupata njia za kuzitatua, baba hiyo ni miongozi mwa barabara kadhaa
zilizojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa
ilani ya CCM na kuwaondolea wananchi kero ya kusafiri kwenye barabara
mbovu. |
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki
ujenzi wa nyumba ya mwalimu kwenye shule ya sekondari Mdandamo wilayani
Songea mjini. |
|
Katibu wa NEC, Itikati na
Uenezi Nape Nnauye akishirikiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wai Ruvuma,
kuondosha gogo kwenye eneo la ujenzi wa Zahanati katika Kata ya Mahilo,
Songea mkoani Ruvuma.
|
|
Wazee pekee wawili walisosalia kati ya waliokuwepo
kwenye mkutano wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere wakati wa harakati za
TANU, mwaka 1957 katika eneo la Matogolo, Songea mkoani Ruvuma, Hashim
Gawaza (92) na Clemence Simon Nyoni (93), wakivishwa vazi la heshima na
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipowasili eneo hilo jana, Nov
19, 2013. |
|
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akiwa na Wazee hao. |
|
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto) akiwa na wanachama wa
Shina namba noja, waliokuwa wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, alipotembelea nyumbani kwa Mjumbe wa Shina namba
moja, Magreth Mtiula, eneo la Mfaranyaki mjini Songea.
|
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
akisalimiana na muasisi wa TANU na baadaye CCM, Mzee Mustafa Songambele,
baada ya kuzungumza na wanachama kwenye shina namba moja mjini Songea |
|
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimsalimia mama
huyu, Mkazi wa mtaa wa Mfaranyaki mjini Songea, baada ya kumuona kuwa
mwenye shangwe kubwa wakati msafara wa Kinana ulipopita karibu na
nyumbani kwa mkazi huyo. |
|
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia baada ya kuzinduliwa shina hilo. |
0 MAOINI :