Posted in
By
danielmjema.blogspot.com
|
Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo
mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto), baada ya
Kinana kuwakabidhi kadi katika kikao kilichofanyika nyumbani kwa balozi Hilda,
Kaya ya Amani Makolo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Zaidi ya wanachama 50
walipokea kadi hizo.
|
|
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
(kushoto) akimpongeza Balozi wa shina, Hilda Komba, baada ya kikao cha
wanachama kilichofanyika kwenye balozi huyo, Nov. 20, 2013, Kata ya
Amani Makolo, Mbinga mkoani Ruvuma. |
|
Kijana Bonus Hyera wa kijiji cha
Lusewa, akimsalimia kwa kumbusu mikono kwa shauku, Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, baada ya Dk. Asha-Rose kukutana na
kijana huyo, wakati wa shughuli ya uzinduzi wa tawi la CCM Kata ya Mbinga
mjini, mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana. Kijana huyo aliyeonekana kama aliyekuwa amelewa kiasi,
alionyesha heshima kubwa kwa Dk. Asha-Rose, tofauti ilivyokuwa inadhaniwa
na baadhi ya watu waliopomuona akimsogelea kwa shauku kiongozi huyo.
|
|
Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake, wakitazama ngoma ya mganda, kabla ya
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa michezo mjini Mbinga
mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. |
|
Wananchi wakiselebuka, wakati wa shamrashamra za kumlaki Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kwenye Uwanja wa Michezo mjini
Mbinga, Novemba 20, 2013. |
|
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi, Nape Nnauye akiliraibu kwa
kulipiga buti, tairi la gari yake kujua kama lilikuwa limetengemaa,
baada ya kupachikwa na dereva wake (hayupo pichani) gari hilo lilipokuwa
limepata pancha katika kijiji cha Lusewa, Kata ya Mbinga Mjini, wakati
msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliokuwa katika kata
hiyo, Nov 20, 2013. |
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na baadhi ya
viongozi katika msafara wake, wakishiriki Nov 20, 2013, kungoa magugu na
visiki, kuandaa shamba la mfano la wanawake na vijana wajasiriamali
katika kijiji cha cha Mkwaya Kata ya Kilimani wilayani Mbinga mkoani
Ruvuma alipotembelea shamba hilo lenye ukumbwa wa ekari 500. Mbali na
kushiriki kazi hiyo Kinana alitoa mchango wa sh. Milioni 4, kwa ajili ya
mafuta ya trekta ya kulimia shamba hilo. Baadhi ya viongozi wengine ni
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro
(kulia).
|
|
Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman akiijaribu pikipiki wakati akikabidhi pikipiki katika awamu ya pili
ya mradi wa pikipiki 50 za vijana waendesha bodaboda kwa mwenyekiti wa kundi la
waendesha bodaboda hao, Alkhass Ramadhani(katikati), wakati wa mkutano wa
hadhara uliofanyika, mjini Mbinga, Nov 20, 2013. Pikipiki hizo zimetolewa na
Mbunge wa Mbiga Mashariki, Ndugu Kayombo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itrikadi na
Uenezi, Nape Nnauye.
|
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akikagua
mradi wa mgodi wa makaa ya mawe wa kampuni ya Tancoal katika eneo la
Mtunduwalo, Mbinga mkoani Ruvuma, Nov 20, 2013. Kinana alitembelea mgodi
huo, kufuatia mgogoro uliopo kati ya wananchi na uongozi wa mgodi
kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo malipo ya fidia kwa maeneo
yalitochukuliwa.
|
|
Balozi wa shina namba 29, Kata ya Amani Makolo, Mbinga,mkoani Ruvuma,
Hilda Komba akifungua kikao cha wanachama, ambacho Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana (kulia) alihudhuria, Nov 20, 2013. Katibu wa
NEC,ltikadi na uenezi, Nape Nnauye (watatu kulia- waliokaa), alihudhuria
kikao hicho.(PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO) |
0 MAOINI :