MWATHIRIKA WA UBAKAJI AKAMATWA SOMALIA
Posted in
No comments
Thursday, November 21, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Sio mara ya kwanza kwa mwathiriwa wa ubakaji kukamatwa baada ya kusimulia yaliomkumba Somalia.Msichana mmoja amekamatwa mjini
Mogadishu Somalia, baada ya kusimulia kituo kimoja cha redio nchini humo
kuhusu alivyobakwa na watu waliomtishia kwa bunduki.
Mwandishi aliyemhoji msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 pia amezuiliwa.Umoja wa Mataifa unataka uchunguzi
ufanywe kuhusu madai hayo ukiwema kuwa unapiga darubini uhuru wa vyommbo
vya habari na ambavyo serikali itachunguza kisa hiki.Serikali ya Somalia inasema kuwa lazima haki itendeke.
Mapema mwaka huu , mwathiriwa mmoja wa ubakaji
pamoja na mwandishi wa habari walifungwa jela mwaka mmoja ingawa
waliachiliwa baadaye kutokana na uamuzi wa kesi ya rufaa.Ubakaji na waandishi wa habari wanaoripoti visa
vya ubakaji au dhuluma nyinginezo za kingono, ni mada ambayo huhofiwa
kuzungumziwa nchini Somalia na kesi hii ndio ya hivi karubui kuhusu
polisi kumkamata mwathiri wa ubakaji pamoja na mwandishi habari
aliyemhoji.
Msichana huyo aliambia kituo cha redio cha
Shabelle, kuwa alibakwa na waandishi habari wenzake wawili wakiwa akiwa
ameshikiliwa bunduki."mmoja alinitishia kwa bunduki na kunipeleka
chumbani kwa nguvu , na kunivamia huku akinivunjia heshima yangu, ''
msichana huyo alinukuliwa na shirika la habari la AFP akisema katika
video kwenye mtandao wa Redio Shabelle.
"ninaomba serikali kuchukua hatua dhidi ya
wabakaji hawa, huenda wamewatendea unyama huu wasichana wengine wasio na
uwezo wa kujitetea,'' alisema msichana huyo.Video hiyo imepeperushwa kwenye mitandao mingine ya habari nchini humo.Polisi walimkamata mwanamke huyo pamoja na
mwandishi wa habari Mohamed Bashir Hashi, aliyemhoji pamoja na mkuu wa
idhaa ya Redio Shabelle Abdulmalik Yusuf.
Hakuna hata mshukiwa mmoja, aliyetuhumiwa amechukuliwa hatua za kisheria.
Hata hivyo, serikali ya Somalia imesema kuwa
ubakaji na dhuluma dhidi ya wanawake ni mambo ambayo hayaruhusiwi hata
kidogo, ingawa haikutamka chochote kuhusiana na kesi hii.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :