![]() | ||
Sista Maria Lubangura wa Mtakatifu Benedict akiungana na mwenzake
kugalagala jana, mbele ya jukwaa, wakati Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kisangu,
wilaya ya Songea Vijijini, na kutangaza kuitisha harambee baadaye kwa
ajili ya kuchangisha fedha ili kusaidia kupatikana fedha kwa ajili ya
kujenga upya Kituo cha Afya cha Masista cha Fabio Chipole,
kilichoteketea kwa moto hivi karibuni. Kulia ni Mbunge wa Peramiho,
Jenista Mhagama.
|
![]() |
| Zena Honde ambaye ni mke wa Balozi wa Shina namba moja, Issa Saidi, akimkaribisha kwenda kunywa chai nyumbani kwa balozi huyo, Katibu Mkuu wa CCM na msafara wake, baada ya katibu Mkuu huyo kuzungumza na wanachama wa CCM katika shina hilo, Nov 19, 2013, mwanzoni mwa ziara yake katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini. |
![]() |
| Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kushoto) na msafara wake wakiungana na wananchi kusomba matofali wakati wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Nakahewa, katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini, jana. Wengine baadhi ya viongozi waliopo kwenye msafara wa Kinana ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro |
![]() |
SIDANGANYIKI: Msichana Magreth Milinga (16) akiwa amevaa fulana
yenye ujumbe wa 'Sidanganyiki' kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa jana
na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika jimbo la Peramiho,
Songea Vijijini.
|
![]() |
| Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizindua Zahanati ya Lusonga, katika jimbo la Peramiho, Songea Vijijini jana. Kushoto ni Ktibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Mbunge wa Peramiho Jenista Mhagama (watatu kushoto). |
![]() |
| Mzee Romanus Joseph (82) mkazi wa Kijiji cha Nakahegwa, Peramiho, Songea Vijijini, akivuta tumbaku, alipokuwa amekaa hatua chache kutoka eneo ambako Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Hayupo pichani) alikuwa akikagua ujenzi wa zahanati katika Kijiji hicho jana, akiwa katika ziara katika Jimbo la Peramiho. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO). |










No comments:
Post a Comment