MAKINDA AMUONYA KAGASHEKI

Posted in
No comments
Tuesday, November 5, 2013 By danielmjema.blogspot.com


SPIKA wa Bunge Anne Makinda amemuonya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki akimtaka ‘kuchunga mdomo wake’ kutokana na kauli anazozitoa nje ya Bunge. 

Hatua hiyo ilitokana na na Mbunge wa Sikonge, Saidi Nkumba (CCM) kuomba mwongozo wa Spika akielezea kitendo cha Kagasheki kutoa matamko mbalimbali kuhusiana na ‘kibano’ alichokipata bungeni wiki iliyopita.
“Ili Spika aweze kutoa ufafanuzi kama jambo hilo linaruhusiwa au haliruhusiwi kwa mujibu wa kanuni, ni juzi tu waheshimiwa wabunge na Bunge lako tukufu limejadili kwa kina suala la dharura juu ya uonevu ambao wamefanyiwa wananchi wetu maeneo mbalimbali wakati wa utekelezaji wa operesheni tokomeza,”alisema Nkumba.

Alisema siku chache baada ya kujadili jambo hilo Waziri Kagasheki alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kwamba wabunge wanasemasema tu ndani ya bunge bila kujali rasilimali za taifa.

Nkumba alisema Kagasheki pia alisema hatishwi na maelezo ya wabunge ya kumtaka ajiuzulu na kwamba hatang’oka madarakani mpaka Rais Jakaya Kikwete aliyemteua atakapomtaka afanye hivyo.

“Yeye mwenyewe ndiye aliyetoa kauli ya kusitisha operesheni tokomeza bungeni… kitendo cha kuwakamata Wachina ni hatua tu ya Serikali ya kila siku ambayo inaweza ikaendelea bila operesheni.

“Waziri katoa nje mambo ya Bunge na kubeza uamuzi wa Bunge na kukejeli Bunge,” naomba mwongozo wako Mheshimiwa Spika kama jambo hili linaruhusiwa.


Makinda alisema: Nadhani kuna matumizi mabaya ya midomo nasema tukishakubaliana hapa halafu kwenda kusemasema huko nje ni kuwasha moto pale ambako moto unawaka vizuri… matamko ambayo si mazuri tuyaepuke”.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .