WAFUASI WA RIEK MACHAR WALA KIPIGO HUKO SUDAN KUSINI
Posted in
afrika mashariki
No comments
Tuesday, April 12, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Waasi nchini Sudan Kusini wanasema
kuwa wanachama wake 16 wa kitengo cha habari, wamekamatwa na kupigwa
vibaya na maafisa wa usalama katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Kundi hilo la waandishi wa habari lilikuwa limetanguliwa katika mji mkuu wa Juba, siku kadhaa kabla ya kuwasili kwa kiongozi wa waasi Dkt Riek Machar.
Dkt Riek Machar anatarajiwa kutawazwa kuwa makamu wa rais kulingana na mkataba wa amani uliositisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoanza Desemba mwaka wa 2013 kati ya waasi wanaomuunga mkono bw Machar na wanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir.
Walikuwa wakijaribu kuwakusanya watu ili kumkaribisha naibu mwenyekiti vuguvugu la waasi, Alfred Ladu Gore.
Hapo jana Jumatatu, zaidi ya waasi wapatao 1,300 walisafirishwa kwa ndege hadi Juba, kama ilivyohitajika katika muafaka wa amani uliotiwa saini majuzi. Walitakiwa kuhakikisha kuwa usalama wa Bwana Machar, ambaye aliteuliwa majuzi kuwa makamu wa Rais, uko sawa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :