UN KUCHUNGUZA WAKIMBIZI WA DABAAB

Posted in
No comments
Tuesday, November 19, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Wakimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya
Umoja wa Mataifa unajiandaa kuanza utafiti kwenye kambi kubwa ya wakimbizi duniani ya Dadaab iliyopo Kaskazini mwa Kenya ili kujua wakimbizi karibu nusu milioni kutoka Somalia waliopo kwenye kambi hiyo ambao wapo tayari kurejea nchini mwao.Wiki iliyopita Kenya na Somalia walitiliana sahihi makubaliano na Umoja wa Mataifa ili kuanza kurejesha wakimbizi hao nchini Somalia.

Mwandishi wa Habari wa BBC aliyepo kwenye kambi hiyo anasema ni wakimbizi wachache chini ya mia moja ambao wapo tayari kurejea nchini mwao, ambapo wengi wanasema hali ya usalama nchini Somalia bado ni hatari kutokana na kuwepo kwa wapiganaji wa Kiislamu.

Kuwepo kwa wakimbizi imezusha wasiwasi wa kisiasa nchini Kenya kufuatia shambulio la Septemba ambapo wapiganaji wanaodaiwa kuwa ni wa Kisomali kushambalia kituo cha biashara cha Westgate ambapo watu 67 waliuawa.Serikali ya Kenya imesema miaongoni wa walioendesha shambulio hilo ni wakimbizi kutoka kwenye kambi hiyo ya Daadab. 
source:bbc swahili

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .