Wacheza kikapu Tanga waomba msaada kuipeleka timu Mbeya.
Posted in
No comments
Sunday, November 17, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
Na mwandishi
wetu
Mabingwa
watetezi wa michuano ya taifa ya kikapu (Taifa Cup) kwa mwaka jana, bado
hawajathibitisha ushiriki wao katika michuano ya mwaka huu kutokana na ukata wa
fedha.
Kwa mujibu wa
vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa mabingwa hao wa mwaka jana ambao ni Mkoa wa
Tanga, mpaka sasa timu yao inafanya mazoezi bila matumaini ya kuelekea mjini
Mbeya itakapofanyika michuano hiyo kwa mwaka huu mwishoni mwa mwezi wa 11.
“Michuano
hii ya kikapu taifa kwa mwaka jana ilifanyika mkoani hapa (Tanga), hivyo ikawa
rahisi kwetu kuweka kambi na kupata mahitaji mengine, ndiyo maana tukaibuka
mabingwa, lakini mwaka huu hali katika kambi si nzuri kwani bajeti inatubana
mpaka sasa hatujui mustakabali wetu,” kilisema chanzo hicho.
Kwa mujibu
wa barua iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa kikapu mkoa wa Tanga
(TRBA), Carlistus Zakaria timu hiyo inahitaji kiasi cha Sh mil 11, ili kuweza
kusafiri mpaka Mbeya. Vilevile kiasi hicho cha fedha kitaweza kuhudumia kambia
kwa malazi na chakula pamoja na vifaa vya michezo kwa muda wote watakaokuwa
Mbeya.
“Timu yetu
ina wachezaji 24 Wavulana na Wasichana pamoja na viongozi wanane hivyo kufanya
idadi ya watu 32, tunahitaji kiasi cha Sh mil 3.5 za nauli kuenda na kurudi, Sh
mil 5.2 za chakula kwa siku zote tutakazokuwa Mbeya pamoja na Sh mil 8.8 za
vifaa vya michezo na fedha za dharura,” ilisema sehemu ya barua hiyo.
Aidha kwa
mujibu wa chanzo chetu cha habari ambacho kimetaka hifadhi ya jina lake mpaka
sasa Mkoa wa Tanga, haujaonyesha nia ya kuwasaidia mbali ya kuwapelekea barua kutoka Shirikisho
la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), ambayo inaweka wazi kila kitu juu ya
ushiriki wetu.
“Kinachotutia
uchungu juu ya kupuuzwa huku ni kuwa, mwaka jana tulipouletea heshima Mkoa wetu
kila mtu alitusifia, lakini hawakujua kama vizuri vyataka gharama. Sasa ili
tuendelee kuuletea vikombe mkoa wetu tunawaomba wadau wa mchezo huu watusaidie
tufike Mbeya.
“Tumeamua
hatuhitaji fedha, hata wakitokea watu wakitudhamini usafiri, wengine wakatupa
vifaa na wengine wakatuhakikishia chakula hatuna matatizo, kikubwa tunahitaji
kushiriki michuano hii kwa hali na mali, tukishindwa kushiriki itakuwa aibu
kubwa kwa mkoa wetu,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo,
kwa mujibu wa barua ya TBF, iliyotolewa Aprili mwaka huu na kutiwa saini na
Katibu Mkuu Msaidizi wa shirikisho hilo Michael Maluwe, imeweka wazi kuwa
Serikali ya Mkoa inawajibika moja kwa moja kuhakikisha timu hizo zinashiriki
michuano ya Taifa Cup.
“Ni wajibu
wa kila mkoa kuhakikisha unawajibika katika maandalizi na kuipeleka timu ya
mkoa kwenye kituo cha mashindano,” imesema sehemu ya barua hiyo na kuongeza
kuwa. “Mambo muhimu ya kuzingatia ni gharama za nauli kwa timu, gharama za
malazi na chakula vilevile usafiri wa ndani, posho na ada ya ushiriki ambayo ni
Sh 100,000.”
Aidha timu
ya kikapu ya Tanga imeweka wazi kuwa mtu binafsi, kampuni ama taasisi ambayo
itaguswa na matatizo ya kambi hiyo, ambayo inapigana kuhakikisha inatetea
ubingwa wake ilioupata mwaka jana wanafungua milango kupokea msaada wowote
utakaowawezesha kuishi mjini Mbeya kuanzia Novemba 30 mpaka Disemba 8 mwaka huu
itakapokamilika michuano hiyo.
Wamebainisha
kuwa wapo tayari kutangaza biashara ya mfadhili yeyote atakayewasaidia ama mtu
aliyeguswa anaweza kuwatumia fedha katika akaunti ya benki namba 4172506984 NMB
Bank (badaraka Branch).
Mwisho
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :