KUSITISHWA KWA OPERESHENI WATOA MWANYA WA MAUAJI YA KUTISHA YA TEMBO TANZANIA

Posted in
No comments
Tuesday, December 31, 2013 By danielmjema.blogspot.com


Maujia ya tembo yameongezeka nchini Tanzania tangia serikali ya nchi hiyo kusitisha Opereshieni tokomeza kutokana na kuwepo madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.Naibu waziri wa Maliasili na utalii nchini Tanzania Lazaro Nyarandu amesema kuwa idadi ya tembo 60 wameuawa katika kipindi cha miezi miwili tu ya mwezi Novemba na Disemba ikilinganishwa na tembo wawili tu waliouawa mwezi mwa kumi mwaka huu.

Hata hivyo idara za ulinzi zilikubaliana kuwaua majangili watakaobainika wakiwaua tembo hao kipindi ambacho msako huo ulikuwa ukiendelea mwezi Oktoba mwaka huu.Hata hivyo serikali ilisitisha operesheni hiyo kufuatia malalamiko kwamba watekelezaji wa msako huo walikuwa wakikiuka haki za binadamu.
 
Waziri mkuu wa Tanzania alikaririwa akisema operesheni hiyo ilikuwa na nia njema lakini taarifa za kuwepo vitendo vya mauajia na ukikwaji wa haki za binadamu ndicho ambacho hakikubaliki na serikali.
 
Hata hivyo matokeo ya uchunguzi wa kamati maalumu kuhusiana na kuwepo kwa ukiukwaji wa haki za binadamu ndiyo uliosababisha Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwafukuza kazi mawaziri ,Shamsi Vuai Nahodha wa jeshi la ulinzi, Emmanuel Nchimbi wa mambo ya ndani,waziri wa Utalii na maliasili Khamis Kagasheki na waziri wa Maendeleo ya Mifugo David Mathayo.

Nchi za kutoka bara la Asia ndizo zinazodaiwa kujihusisha Zaidi na biashara ya pembe za ndovu hali inayoongeza kasi ya ujangili na mauaji ya tembo nchini Tanzania

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .