RAIA WA BURUNDI ANAYETUHUMIWA KUMILIKI MTANDAO WA KUSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU ANASWA KILIMANJARO
Posted in
No comments
Friday, December 20, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
IDARA ya uhamiaji Mkoani Kilimanjaro, kinamshikilia Mtu mmoja, Raia wa
Burundi anayedaiwa kuwa Kiongozi wa Mtandao uliohusika kusafirisha
wahamiaji haramu zaidi ya 76 kutoka Ethiopia kuigia ndani ya Nchi,
kupitia eneo la Tarakea linalounganisha nchi za Kenya na Tanzania.
Mtuhumiwa huyo, Abdulkadir Ndayeshimiwe (33), mwenye hati ya kusafiri ya nchi ya burundi, namba OP0024157, alikamatwa juzi, katika ofisi za Uhamiaji Tarakea akiwa anajaribu kukapata kibali cha kusafiri kuingia nchini akitokea Loitoktok nchini Kenya, akielekea jijini Dar es salaam.
Taarifa ziliztoka ndani ya Ofisi za makao makuu ya idara ya uhamiaji mkoani Kilimanjaro zinadai, kuwa Ndayeshimiwe ambaye ni mtuhumiwa muhimu katika tukio la kukamatwa kwa Wahamiaji haramu 11 pamoja na wengine 56 mkoani Kilimanjaro lililotokea hivci karibuni aliingia nchini katika jaribio la kutaka kumuokoa Mburundi mwenzake aliyekamatwa katika tukio hilo.
Taarifa hizo zilisema kuwa, Ndayeshimiwe (pichani) alikuwa katika jaribio la kutaka kufanya juhudi za kumtoa hatiani, Paul Nduwayesu, aliyekamatwa Desemba 16, majira ya saa 1:15 mchana akiwa na Wahamiaji Haramu 10 katika Nyumba ya kulala wageni cha Impala, iliyopo Tarakea wilayani Rombo.
Inadaiwa kuwa Mtuhumiwa huyo ambaye ni mzaliwa wa mji wa Kayanze katikati mwa Burundi na Mfanyabiashara wa vifungashio vya Plastiki, kutoka Tanzania na Kenya kupeleka nchini Burundi, amekuwa akifanya biashara ya Kusafirisha Wahamiaji haramu wengi kutoka katika Nchi za Ethiopia na Somalia ambapo anashirikiana na Watanzania wanaokaa katika maeneo ya mpakani.
Akiungumza na Waandishi wa Habari, Ofisini kwake, Mkuu wa Idara ya Uhamiaji mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Johannes Msumule alisema baada ya kupata taarifa za ushiriki wa Mtuhumiwa huyo katika Biashara hiyo kutoka kwa Nduwayesu, Uchunguzi ulianza mara moja ambapo, Desemba 19, walifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa huyo.
Msumule alisema kukamatwa kwa Ndayeshimiwe aliyekamatiwa katika Ofisi za uhamiaji Tarakea, kulitokana na ufuatiliaji wa makini ambao ulibaini kuwa amekuwa akifanya mawasiliano na Watuhumiwa wawili waliokamtwa siku chache zilizopita akiwemo Mmiliki wa Gesti ya Impala, Leokadia Tarimo ambaye naye yuko mikononi mwa Jeshi la Polisi.
Msumule alisema baad ya mahojiano, Ndayeshimiwe alikiri kufanya biashara hiyo na kwamba katika maelelzo yake alieleza namna ambavyo alikutana na watuhumiwa wengine wawili, Nduwayesu Paul na Leokadia Tarimo kupanga mikakati ya kusafirisha na kuhifadhi wahamiaji 10 katika Gesti ya Impala.
Aidha Mkuu huyo wa Uhamiaji mkoani hapa alisema mbali na maelezo ya Mtuhumiwa huyo, waliweza kufanya upekuzi katika simu yake na kugundua amekuwa akifanya biashara hizo kwa msaada wa Mtanzania mmoja mkazi wa mji wa Moshi, ambaye alimtaja kwa jina moja la Dulla.
Alisema kwa sasa Jeshi hilo linaendelea kufanya Uchunguzi kuweza kubaini alikojificha Dulla na kwamba zaidi ya hayo Maaskari wa Uhamiaji wanaendelea kufuatilia mawasiliano yanayoingia kwenye simu hiyo kuona kama kuna Vigogo wa serikali au kutoka katika Idara yake au Jeshi la Plisi ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakimsaidia Mtuhumiwa huyo na mtanadao wake.
Msumule aliongeza kuwa katika hati ya kusafiria ya Mtuhumiwa huyo waliweza kubaini kuwa Ndayeshimiwe pamoja na kuwa ni Raia wa Burundi ana muda mrefu hajafika katikia nchi yake kwani taarifa zinaonesha kuwa makazi yake kwa sasa yako nchini Kenya katika Jiji la Nairobi.
“Kama nilivyoahidi kuwa tutapigana kufa na kupona kuhakikisha Kiongozi wa Watuhumiwa wale wawili tunamtia nguvuni, Jana, tulifanikiwa kumkamata, Abdulkadir Ndeyashimiwe, mkazi wa Kayanze, Burundi, ni Mfanyabiashara wa Plastiki kutoka Kenya na Tanzania kwenda Burundi, lakini mbali na biashara hiyo tumabaini, mtu huyu ni msafirishaji mkubwa wa wahamiaji haramu, alikamatiwa pale Tarakea uhamiaji”,
alisema Msumule.
Kwa upande wake, Ndeyashimiwe akitoa sababu za yeye kuingia Tanzania, alisema amekuja nchini baada ya kupokea simu kutoka kwa Mdogo wake, Nduwayesu Paul aliyekamatwa na Jeshi la Polisi, ambaye alimpa taarifa za kukamatwa kwake.
Alisema alipoingia nchini alikuwa najaribu kufanya utaratibu wa kufahamu sababu za kukamatwa kwa mdogo wake na sio kweli kwamba anahusuika na biashara hiyo kama inavyodaiwa na kwamba pale Tarakea alikuwa anatafuta kibali cha kumruhusu kufanya safari ndani ya nchi ambapo alikuwa anaeleka Dar es salaam.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :