TCRA YAIWASHIA TAA YA KIJANI AZAM TV

Posted in
No comments
Friday, December 6, 2013 By danielmjema.blogspot.com

Azam Media Ltd  leo imepata leseni kutoka Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA) na hivyo kuwa na uwezo wa kuanza rasmi shughuli zake hapa Tanzania.

Hatua hii muhimu sasa inaiwezesha AzamTV kuanza kutoa huduma zake kwa wateja wake kote Tanzania kuanzia tarehe16 Desemba. Huduma hii itwapa fursa wateja kuangalia zaidi ya chaneli 50 za kitaifa na kimataifa ziliozosheheni burudani kwa ajili ya familia kwa bei nafuu ya shilingi 12,500/= kwa mwezi. 

Kutakuwepo wigo mpana wa kuchagua kifaacho kuangalia vikiwemo vipindi vya michezo, makala, watoto na tamthilia kutoka Tanzania, barani  Afrika na sehemu mbalimbali za dunia. Baadhi ya vipindi hivyo tajwa vitapatikana katika chaneli maarufu  kama vile National Geographic Gold na Nickelodeon, na pia matangazo yetu yatakuwa na chaneli za bila malipo zikiwemo TBC1, Channel 10, Clouds, ZBC na K24.

Jambo la kusisimu zaidi  ni kwamba  AzamTV itakuwa na matangazo katika chaneli zake tatu:
AzamOne - Itakuwa na vipindi vya kiafrika, ambapo kwa asilimia kubwa vitahusu masuala ya Afrika Mashariki kwa lugha ya Kiswahili. Hii ndiyo chaneli ambayo itakuwa ikirusha matangazo ya Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara;

AzamTwo – Hapa vitapatikana vipindi vya burudani kwa familia amabavyo ni vya kimataifa na baadahi ya hiovyo vitakuwa katika lugha ya kiswahili;Sin emaZetu – Chaneli maalum kwa ajili ya tamthilia za kitanzania.

Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema: “Huu ni  wakati wa kujivunia  kwa Tanzania kwani sasa ina huduma za luninga zinazopatikana kwa  bei ambayo wengi wanaweza kuimudu.  Miezi michache ijayo tutaivusha huduma hii mipaka hadi katika nchi zingine za Afrika Mashariki na hata mbali zaidi. Nimefarijika kwamba tumewekeza vilivyo katika chombo hiki cha kitanzania na tutaendelea kufanya hivyo”.

Torrington pia alibainisha kuwa kwa wateja ambao hawatapenda kungojea kuzinduliwa rasimi wa huduma za Azam TV, milango ya ofisi zake za Dar es Salaam itakuwa wazi kuanzia  leo (Ijumaa Desemba 6, 2013).  Wateja wataweza kununua  vifaa muhimu kutoka duka la AzamTV na kwa mawakala walioidhinishwa  na hivyuo kuweza kujionea vipindi mbalimbali kuanznia sasa – japo malipo yao kwa mwezi yatahesabiwa kuanzia Desember 16.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .