WAZO LA LEO: MAWAZO YA MDAU WA TAIFA LETU.com KUHUSU WASANII WA KIBONGO
Posted in
No comments
Wednesday, December 18, 2013
By
danielmjema.blogspot.com
patty a.k.a Hakunaga |
Hakuna kitu kizuri katika kazi au maisha
kama nidhamu
ambayo inakuongoza kwa kila ufanyacho ,huwa naamini nidhamu ni mtaji
(msingi )mkubwa sana katika maisha ya binaadamu ikifuatiwa na mitaji
mingine kama ya kifedha
,mali , na mingineyo. nimekuwa nikiandika
katika ukurasa wangu wa facebook juu ya wasanii ambao wanapata mafanikio
nakusahau wale wadau au watu wao
wakaribu waliowafikisha mahali walipo hii leo au kuwafanya kujulikana
kwa namna moja ama nyingine .
wasanii
wamekuwa
wakipokea lawama nyingi sana
toka kwa wadau mbalimbali hasa waliopo katika kiwanda kimoja cha
kiburudani naamaanisha (watangazaji )
mashabiki wao na watu wengineo. wasanii
wanapokuwa hawajatoka wanapokuwa katika
utafutaji wa nafasi za kufahamika ,
wamekuwa ni watu ambao kwa namna moja ama nyingine wakihangaika sana na
watangazaji , bloggers au wamiliki wa vyombo vya habari hapa nchini kwa
lengo la kuomba kupewa muda hewani, kutambulishwa kwa wadau , au
kupigiwa ngoma wanazotoa au video
walizonazo.
naweza nikasema ni watu
ambao wamekuwa wakitumia akili nyingi
sana, nguvu nyingi sana na hata wakati
mwingine kutumia kiasi cha fedha ili tu kufanya kazi zao au wao wenyewe
kufahamika , na hii sio tu kwa wasanii wa
muziki , hapana , hata wasanii
waliopo katika kiwanda cha filamu hapa nchini.
nashindwa
kujua tatizo la kujisikia , kuwa na
dharau pamoja na kuweka mipaka ya kuongea na baadhi ya vyombo vya habari au
watangazaji kwa hawa wasanii wetu ni
ulimbukeni, ujuha, ustaa au kulewa sifa ?????
kuna
baadhi ya wasanii ambao ukiangalia
mwanzo wakati wanatoka na walivyokuwa wanasumbua watu kwa namna moja ama
nyingine , unaweza pata hasira na
kujikuta kujuta
WHY ULIMSAIDIA KIPINDI KILE , NA KWANINI
HUKUMUACHA ???
Na hii ni kutokana na
tabia ambazo wamekuwa wakizionyesha wakati mwingine. baadhi wamekuwa
na dharau , wamekuwa wakutokujali ,
wamekuwa kitu kingine kabisa tofauti na mwanzo au tofauti na alivyokuwa
.
hapa ndipo tunapojiuliza kuwa kwani
kupata mafanikio, kujulikana, kusikika, au kuonekana , ndo njia ya kumfanya mtu
abadilikie, anate, ajishaue shaue , au
nini?? is it true that mafanikio ni
sehemu ya kumbadilisha mtu kweli katika maisha???? yaani anapopata mafanikio tu
ni lazima mtu utoke katika uhalisia wa tabia njema, ucheshi au upendo uliokuwa nao na ubadilike uwe kitu
kingine kabisaaa kisa ni MAFANIKIO??? basi mafanikio ni shetani, kwa maana
nyingine au ni nini??? maana kama MAFANIKIO
tafsiri yake ni nzuri basi tusingefika huku au kuwa na mambo kama haya ,
au MAFANIKIO NI MARINGO??? labda yaweza kuwa sijui tafsiri ya mafanikio,
nisaidie tafadhali.
mimi
naamini maisha ni jinsi unavyotaka kuyaishi wewe kama wewe au kujipangia mtindo
wako wa maisha unaotaka kuishi lakini pia katika kupanga mtindo huo wa
maisha lazima uwe na tahadharai kwamba
maisha haya ninayoyaishi au ninayotaka kuyaishi yasiniongezee maadui na
badala yake yaniongezee marafiki angalau kwa asilimia chache au kubwa zaidi .
ni
wazi wasanii wetu juu ya hili ( waliopo
katika filamu, na waliopo katika muziki )
wanakosea sana kwa wale
baadhi wanaofanya haya , yaani baada tu
ya mafanikio anakuwa ni mtu wa dharau,
majivuno, nk.kwa namna moja ama nyingine nakusahu alipotoka na anapoelekea ..
naamini siku mtu mwenye mafanikio yake ( kimuziki ,)
akirudishwa nyuma hata kwa dakika kumi kumuonyesha alivyokuwa anaomba
au kulia kwa kunyenyekea juu ya kazi zake kupata air time kwa
watangazaji au wamiliki wa
vyombo vya habari au alivyowapigia goti
mashabiki kumuwezesha kufika alipofika anaweza kuanguka kifafa au kukataa kabisa kuwa siyo muhusika au sio yeye .
Nimefanya
vipindi vingi vya kiburudani kwa muda mrefu , na nimekuwa niki experience
hali hii kwa muda mrefu toka kwa
wasaniii wa filamu na wasanii wa
muziki hapa nchini .nimekuwa
nikijifunza pia kupitia kwa hawa wasanii wetu na pia kujikosoa mwenyewe na hata
kuwakosoa hao kwa kile ambacho naona hakipaswi kuwa hivyo kilivyo katika kiwanda hiki cha kiburudani .
Wasanii
wetu wa kitanzania wengi wao wamekuwa
wakijiaminisha kuwa dar es salaam ndo kila kitu na kwa media zilizopo huko ndo
kila kitu yaani bila hizo media wao hawajatoka.
wasanii wetu wa kitanzania wamekuwa wakiamini mashabiki wakubwa wao ni
mashabiki wa Dar tu.
wamekuwa
pia wakiamini watangazaji
wakuwatoa ni watangazaji waliopo Dar tu
na si kwingineko, vitu ambavyo ninavipinga
hadi mwisho wa pumzi yangu!!!
ni
wasanii wangapi wameanza kujulikana mikoani kabla ya dar??? ni wasanii wangapi
wanapata air time ya kutosha kutoka katika radio za mikoani tofauti na
radio za dar?? ni wasanii wangapi
wamekuwa wakipigwa kazi zao bureeeeeeeeeeeeeeeeeee pasipokulipa chochote na
radio za mikoani tofauti na Dar???
ni
wasanii wangapi wamekuwa wakipewa interviews
na radio za mikoani pamoja nakutambulishiwa ngoma zao tofauti na
dar??? kama ulikuwa hulitambui hili fanya utafiti utanipa JIBU .
NI wengi mno
ambao hadi kesho wanashukuru radio za mikoani zilizowatoa na kuja baadae kujulikana dar. lakini swali
langu bado ni lile lie kuwa baada ya
hapo sasa je MAFANIKIO NI DHARAU KWA RADIO ZA MIKOANI NA MASHABIKI WA MIKOANI
?????? AU MAFANIKIO NDIO CHACHU YA KUONGEZA
MASHABIKI ???? utajijibu
mwenyewe............!
wasanii
lazima wabadilike na wajifunze kuwa kama walivyokuwa mwanzo, maana
wengi wao wanapopata kufahamika tu , dharau zinakuwa nyingi sana ,
wakati mwingine simu hawapokei , ukiomba kuwa na interview nao ni shida,
yaani kiukweli hapana baadhi ya wasanii wanachosha. HAKUNA ANAYETAKA
KUABUDIWA , LAKINI JARIBU KUJALI NA KUTHAMINI WALE WANAOCHANGIA
KUKUFIKISHA MBALI AU MAHALI ULIPO , MAANA NAAMINI WANGEAMUA KUWA
AMBAVYO UPO AU KUKUONA WANINI KIPINDI AMBACHO UNAHANGAIKIA KUWAOMBA
KAZI ZAKO ZIPIGWE AU WAKUPE INTERVIEW , NI WAZI UNACHORINGIA LEO
KINGEKUWA NI HISTORIA.
Baadhi yenu mnakera!!!!!.
MANENO YANGU SI SHERIA , WALA MSAHAFU AU BIBILIA YANAWEZA KUKOSOLEWA TU PALE AMBAPO NIMEKWENDA TOFAUTI .
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :