CHADEMA YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UDIWANI ARUSHA TANGA, NA KILIMANJARO
Posted in
No comments
Friday, January 17, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
TAARIFA WA UMMA
WAGOMBEA WA UDIWANI – KANDA YA KASKAZINI
Tarehe 15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa
na TUME YA UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo
ya kata mbalimbali za kanda ya Kaskazini.
Wagombea hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina
matarajio makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi
watapata fursa nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana
dhamira njema sana na ya kweli katika kuwatumikia.Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
JINA LA MGOMBEA
|
KATA
|
JIMBO
|
MKOA
|
BI. MWANAISHA MOHAMED OMARI
|
KIOMONI
|
TANGA DC
|
TANGA
|
BW. KAGOMA FRANK HENRY
|
KIBORLONI
|
MOSHI MJINI
|
KILIMANJARO
|
BW. ALLY BANANGA
|
SOMBETINI
|
ARUSHA MJINI
|
ARUSHA
|
BW. CHARLES SAMWEL MGATA
|
PARTIMBO
|
KITETO
|
MANYARA
|
BW. SANING’O KONE
|
LOLERA
|
KITETO
|
MANYARA
|
Katika uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana
tukiwa na uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao
kwa kuzingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana
na kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za
wananchi zilizoletwa na CCM kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.
Aidha chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa
kumteka mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya
tarehe 15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa.
Tukio hili limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa
mida ya saa nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM
wa wilaya.
Uongozi wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba
LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI
JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia
barua msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na
kupotea kwa mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili
kwa kina chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.
Hivi sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa
kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili
ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia
ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka.
Niwahakikishie wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko
ambao jambo hili limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa
mpaka apatikane akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea
na pia awaeleze watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini
nyuma yake. Hapa kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili
jambo halitaisha kirahisi hivi hivi.
Niwaombe wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu
tuunganishe nguvu zetu kwa sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na
rasilimali zetu, ili tuwashughulikie CCM ambao wamekuwa wakiendelea
kuwatesa Watanzania kwa sera zao mbovu na uongozi wa kihuni ambao
haujali kabisa maisha ya Watanzania.
Imetolewa na Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini
+255 754 912 914 au 0784 343 275
golugwa@gmail.com
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :