KUTOKA FACEBOOK.....SABABU TANO ZA EDWARD LOWASSA KUWA RAISI 2015

Posted in
No comments
Sunday, January 19, 2014 By danielmjema.blogspot.com




MTOA MADA: Niliwahi kutoa ahadi kuwa nitaweka sababu nzito Tano ambazo mimi binafsi naziona zinafaa sana kumtathmini Edward Lowasa kama Rais ambae Tanzania inamuhitaji kwa muongo mwingine ujao.

Nikiri wazi kwamba kwa CCM ni Lowasa pekee mwenye sifa hizo labda nitamlinganisha na Dr. Slaa ambae kwa muono wangu kidogo anamkaribia Lowassa nikimaanisha kidoogo wanalandana na nitasema wapi Lowassa anampiku Slaa.

Kwa utangulizi tu ni kuwa Nchi hii ili iendelee inahitaji KIONGOZI kwa ufupi kabisa niseme hivyo inahitaki KIONGOZI SHUPAVU tena SHUPAVU KWELIKWELI sio masihara.
Waziri mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Monduli Erdward Lowassa.

Tupo kwenye umaskini mkubwa,watu wanateseka bila sababu ya msingi. Vijana tunashabikia tuu kama wehu, wengine ni wasomi lakini tunapelekwa kama upepo tukisikia hiki "hewala" tukisikia kile "sawa" tukiambiwa hivi "alhamdulilah" tukiambiwa kile "poa tu".
 
Hatutaki kuchambua na kuielewa siasa kwamba kwenye siasa kuna majungu, fitna, kuchongeana, uchu wamadaraka na mali na mambo meeeengi ambapo msipokua makini mnaweza KUMCHUKIA MZURI MKAMPENDA MBAYA.

kwa misingi hii ninaanza uchambuzi wangu. Na uchambuzi huu nitauandika kwa facts and figures kamaanavyosemaga Prof.Muhongo.


1.LOWASSA NA "BIG RESULTS NOW".
 
Nianze na hili.Tunajua wote kuwa serikali yetu sasa ipo kwenye mpango wa matokeo makubwa sasa BRN. Mpango huu mbali na mambo mengine unahitaji kiranja mkuu (RAIS) ambae ni SHUPAVU,JASIRI, MTHUBUTU,MWENYE KUWEKA MALENGO NA KUSIMAMIA KUONA YANATEKELEZEKA lakini pia kama jina la mpango lenyewe lilivyo "MATOKEO MAKUBWA SASA" yaani we want things to happen now.

Kwa minajili hiyo ni kiongozi gani mnaeona anaeweza kuleta matokeo makubwa sasa?embu tuwe wakweliLOWASSA tunamjua alipoingia kuwa waziri mkuu alitangaza kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitano ambacho angekuwa WAZIRI MKUU angetaka kata zote ziwe na shule za sekondari. Sote ni mashahidi alivyosimamia sera hiyo shule zilianza kumea kama uyoga yaani kama mazingaombwe.

Hata maeneo kama ya Kinondoni ambapo ardhi huuzwa kiholela hivyo ardhi kutopatikana lakini ilipatikana kuanzia vijijini hata miji wananchi walianza kujenga shule.ni mashahidi kama sio fitna za yeye kupelekea kujiuzulu sijui leo kielimu tungekuwa wapi.

HE HAD A MASTER PLAN OF OUR EDUCATION SYSTEM AND HE LEFT WITH IT BUT STILL HE HAS IT IN HIS HEAD.
 
Naamini huyu mzee akipata nafasi tutafika. Si hilo tu tunajua mambo mengi aliyokuwa nayo kichwani ambayo mengi yapo kwenye huu mpango ni shupavu ambae angeweza na anaweza kuyasimamia yatekelezeke. Dr.Slaa ni mzuri wa kusimamia mabo lakini somtimes huwa analoose focus nitaliongelea kwenye point ya tatu.
2.LOWASSA ANAJUA KUWEKA VIPAUMBELE NA KUJUA TUNAVIFIKIAJE.
 
Jamani Nchi hii ili iendelee na ndivyo hata nchi zilizoendelea zilivyoanza ni kuwekeza katika elimu ya watu wake, Kilimo na Viwanda nikimaanisha sekta ya uzalishaji. Tunajua jinsi LOWASSA alivyo anza na hayo shule za kata nilishazizungumzia na mipango mingi ya elimu ukitaka kuijua waulize walimu alipoanzisha program ya kuwajengea nyumba,alivyoanzisha program ya kuhakikisha watoto hawakai chini kila mtoto akae kwenye dawati,alivyoshusha ada n.k 

Tusisahau kwenye kilimo aliyoanzissha kilimo cha umwagiliaji mpaka akataka kuleta Mvua ya kutengenezawa mimi huwa nasema hata kama isingewezekana lakini inaonyesha ile nia njema aliyonayo mzee huyu.

Ukitaka kuelewa vizuri waulize wakulima wakuhadithie jinsi alivyokua anawatimua kazi na kuwashtaki watu waliokua wanakula hela za mbolea za ruzuku. Jinsi alivyokua anatafuta masoko ya nje ya mazao ya kilimo waulize wafanyabiashara wakuhadithie.

Ni kiongozi nani mwenye hulka na kariba hii ndani ya CCM? Tunajua wote kuwa mapinduzi ya kilimo na viwanda ndiyo yaliendeleza bara la ulaya historia inatuambia hivyo na elimu ndiyo imeikomboa JAPAN na nchi nyingine LOWASSA ni jenmbe katika hili ana master plan ya mambo haya na anajua kusimamia haya sio siri wala kumpigia debe HE IS REAL.

3.LOWASSA SIO MTU WA KUPOTEZA UELEKEO (TO LOOSE FOCUS)

Lowassa siku zote akitaka kitu ni mpaka kitimie na kikishindikana basi ujue kumpata wa kukiweza ni shughuli pevu na akitaka kitu hakati tamaa idimradi kiwe ni chema hata kama hakina maslahi kwake na ikitokea yeyote akasimama mbele yake kumzuia basi ama zake ama za huyo mtu. wazungu wanasema "You are either with me or against me".

Tunakumbuka jinzi alivyokua akitimua viongozi waliokuwa wakitaka kumkwamisha kwenye utekelezaji wa shughuli za maendeleo. Hakujali urafiki wala nini anakuweka ukimzingua anakumwaga THAT IS THE TYPE OF THE PRESIDENT WE WANT kwa sifa hii hana tofauti na Dr. Slaa japo Slaa huwa wakati mwingine anapoteza uelekeo.

Mfano mzuri wa kutopoteza uelekeo ni kwamba mwaka 1995 alitaka kuwa Rais wakatoswa,2005 akakubali swahiba wake achukue lakini akabaki kuwa focused, fitna zikajengwa akajiuzulu 2007 lakini hata sasa bado hajaloose focus japo anaface a lot of challenges.

Sio mfano mzuri sana huo kutoa lakini inaonyesha ni mtu wa namna gani kuwa siku akitaka vijana tukimaliza vyuo tupate kazi maana yake atalisimamia hilo by hooks or crooks kama ni viwanda kufufuliwa vitafufuliwa idimradi tu vijana tulambe ajira THAT IS THE PRESIDENT WE WANT. A FOCUSED MAN

4.LOWASSA NI HALF DICTATOR HALF DIPLOMATIC

Hahahahaha nianze kwa kucheka maana tunajua hakuna nchi iliyoendelea kwa kiongozi kuwa full diplomatic yaani kitu kidogo "Tume iundwe" jambo dogo "NJOO MEZANI TUONGEE" kitu kidogo "TUSUBIRI UCHUNGUZI" jambo kidogo "DUNIA ITATUELEWAJE". jamani tunamjua.
 
Lowassa ni mtu wa action kwa kwenda mbele Ghorofa limeanguka nani mkandarasi piga chini. Halmashauri imekula hela za maendeleo nani mkurugenzi piga chini. Wizara inatokota nani muhusika piga chini. Tunatatizo fulani solution ni nn tekeleza.yaani hakuna longolongo.Hii ndio type ya uongozi itakayotukomboa Tanzania.
 
Na ukitaka kujua faida yake waulize wachina yaani watakwambia vizuri udictator kidogo unavyoharakisha maendeleo yao. Hakuna TANZANIA hii viongozi wa type hii mbali na LOWASSA na Dr. SLAA tatizo SLAA ....(nitamuongelea wakati mwingine)
5.LOWASSA ANASIKILIZIKA, ANAFUATILIA, SI KIGEUGEU NA SI MVIVU.
 
Hii ni sifa kubwa kwa mtu kuwa RAIS unapoona unataka kuwa Rais au unamchagua mtu ambae kwa haiba yake tu hasikiliziki ujue unaturudisha nyuma.
 
Rais anatakiwa awe akisema hili lifanyike huyo anaeambiwa linamuingia moyoni. Nirudie Rais anatakiwa anapoongea hata kwa simu tu ile pitch ya sauti iashirie kuwa jambo hili ni lazima lifanyike.Yaani kama anaongea mbele yako ukimwangalia kuanzia nywele mpaka unyayo uashirie kuwa kiongozi anataka hili lifanyike.
LOWASSA yupo hivyo akisema jambo linatekelezwa na haiishi hapo anafatilia mwanzo mwisho si mvivu hata kidogo.kutwa anaizunguka Tanzania hii vijijini hadi mijini nyote ni mashahidi wa hili.

HAYA NI BAADHI YA COMMENTS ZA WASOMAJI WA FACEBOOK....SIMAMA SASA NA UHESABIWE 


  • 4 people like this.
  • Evance Komba toa weu wewe
  • Abdullah Bakari Junior Mhhhhhhhhh umejitahid kumfagilia huyu jamaa bt bdo kwa upande wng bdo kabisa huyu jamaa anaua kimya kimya hana lolote na hafai kuwa rais hata kidogo...2kimpa urais 2meisha.......we jamaa fanya mpango uende kwake akupe kaz ya kukpigia kampn sawa eeeeh.........wa2 tunamjua lowasa zaid unavyomjua ww.........
  • Emmanuel Khonga Watu wanatumia nguvu sana kumpinga LOWASA, kuna nini??? ana haki kikatiba kugombea URAIS wekeni nanyi mtu wenu tumjue.
  • Abdullah Bakari Junior Humu ndan kuna wa2 wana makamac kwenye vichwa vyao km huyu emma............
  • Emmanuel Khonga Lete hoja usitukane, matusi yanawakilisha nafsi yako, hujitambui.....nina haki kikatiba na si kuchaguliwa au kuongozwa na fikra zako. NB: badilika au vua hilo vazi takatifu ili utukane vizuri Abdullah Bakari Junior
  • Mgoma Kufa Ila lowasa amesababisha hadi leo kila kukicha umeme unapanda? mie naona tukubali liwalo na liwe tuchague chama pinzani tuone upepo wao ukoje. kitu slaa anafaa
  • Emmanuel Khonga Ukitoa LOWASA kuna Mwakyembe na Magufuli ambao wanafanya kazi kwa vitendo, tumedanganywa sana. Kama nchi yetu kuibiwa ilishaibiwa sana na watu hawafanyi lolote la kukumbukwa, sipendi kuenda kiundani zaidi ila tumwache LOWASA afanye yake 2015 halafu wat...See More
  • Abdullah Bakari Junior Ooooooooo sorry bro ila hiz propaganda zko zinatia hacra coz huyu jamaa kafanya mambo mabaya meng 2 na kaichafua sna nch pamoja na chama ana2mia pesa zko kuwarubun wa2....achana nae huyu jamaa co bro@emma.........
  • Emmanuel Khonga Kuna watu tunawaamini hawatufikishi kwenye matarajio yetu, wakati nchi ina kila rasilimali, hivyo tuwaache kila mmoja aje na sera zake, kuna wengi sana wanatumia njia kama anayotumia LOWASA ila wakizidiwa wanataka huruma za sisi wananchi lakini utendaj...See More
  • Shadrack Mwamaso Bodaboda goo...!bruuututututu... Mtoa mada umepewa Boxer, toyo, Sanlag au uko vikoba? Tehe
  • James Laiser Ni heri umesema kuwa unatoa sababu tano ambazo wewe "BINAFSI UNANADHANI" kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais!

    Kwa kuwa ni sababu zako "binafsi'na sio za watu wengine,ni haki yako kuendelea kudhani km ulivyosema lakini sio Watanzania wanasema.
    ...See More
  • Simon Reuben Alipokuwa wzr mkubwa LOWASA kapitisha mikataba feki na wenzake na kutufanya leo umeme uko juu baada ya deal na nduguye Rostam. Umpe urais si tutauzwa wote.@ Emma badilika
  • Emanuel Goodluck Kant ukishakua na kashfa hufai kuongoza nchi.
  • Doris Shangwe Komu maneno mengi umeandika bt yote n pumba hafai

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .