MAMA SALMA KIKWETE JANA ALIFUNGUA MKUTANO WA MAJADILIANO KUHUSU KUTOKOMEZA VVU KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO
Posted in
No comments
Wednesday, January 22, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa rasmi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, kwenye hoteli ya Serena alikoenda kufungua
mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi
vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Mheshimiwa Mama Zakhia Meghji, Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, (kushoto), wakielekea kwenye chumba cha
mkutano.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano
wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya
virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto uliofanyika kwenye
hoteli ya Serena.
Dr.
Khadija Mwamtemi kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, alikuwa ni
mmojawapo kati ya washiriki waliochangia mawazo yao mara baada ya mada
mbalimbali kutolewa.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu
kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa
mtoto wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo
pichani). Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es
Salaam tarehe 21.1.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :