RAIS MALINZI MGENI RASMI TUZO ZA MAKOCHA BORA MACHI 8 DAR ES SALAAM.
Posted in
No comments
Thursday, January 23, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya tuzo ya makocha wa mpira wa miguu Tanzania inayotarajia kufanyika Machi 8, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya tuzo ya makocha wa mpira wa miguu Tanzania inayotarajia kufanyika Machi 8, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mtandao huu jijini Dar, Afisa Mtendaji wa tuzo hiyo, Fredrick Luunga alisema
kamati ya maandalizi ya tuzo iliyokutana hivi karibuni ndiyo iliyopitisha jina
la Malinzi kuwa mgeni rasmi siku hiyo.
Luunga alisema
lengo la kumwalika kiongozi huyo wa juu wa soka ni kuthamini mchango wake katika
kuendeleza mchezo huo hapa nchini na pia kumpa fursa ya kukutana na kuzungumza
na makocha wa mpira wa miguu Tanzania na wadau wengine kupitia hafla hiyo.
Kuhusu
maandalizi ya tuzo hiyo kiujumla, afisa huyo alisema yanakwenda vizuri na
kwamba wapo katika mchakato wa kutafuta wadhamini zaidi.
“Maandalizi
yanakwenda vizuri na kamati imekuwa ikikutana mara kwa mara kwa lengo la
kupanga mikakati mbalimbali”, alisema.
Hata hivyo,
Luunga ametoa wito kwa wafadhili wa michezo nchini kujitokeza na kudhamini tuzo
hiyo itakayokuwa ikitolewa kila mwaka.
“Bado
tunahitaji wafadhili zaidi ili kufanikisha utoaji wa tuzo hizo kwani lengo ni
kuhakikisha makocha wa soka nchini wanathaminiwa kutokana na kazi zao
wanazofanya katika taaluma ya ukocha”, alisema.
Wakati huo
huo, afisa huyo alisema zoezi la kuwapigia kura makocha wanaostahili kupata
tuzo hizo linaendelea kwa kuandika
katika simu neno sokafasta acha nafasi kisha jina la kocha yeyote na tuzo
anayostahili kupata kisha itumwe kwenda 15678.
Tuzo zinazotarajiwa
kutolewa siku hiyo ni kocha bora wa mwaka 2013, kocha bora wa makipa, kocha
bora mkongwe mwenye mafanikio makubwa, kocha bora chipukizi, kocha bora wa
kike, kocha bora wa kigeni, kocha bora wa kigeni aliyewahi kupata mafanikio
makubwa nchini na kocha bora Mtanzania anayefundisha soka nje ya nchi kwa sasa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :