By
danielmjema.blogspot.com
|
Wajumbe
waMkutano mkuu wa CCM wa uchaguzi wa jimbo la kigamboni wakiwa wenye
nyuso za furaha siku ulipofanyika uchaguzi huo kwenye ukumbi wa chuo cha
Mwalimu Nyerere, Kigamboni. |
|
Mgeni rasmi
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Ndugu Yahaya Sikunjema
akifungua rasmi mkutano wa CCM wa uchaguzi wa jimbo la kigamboni mbele
ya Wajumbe wa mkutano huo. Kutoka kushoto kwenye meza kuu ni Mbunge wa
Jimbo la Kigamboni Ndugu Faustine Ndugulile, Katibu wa wilaya Temeke,
Ndugu Robert Kilenge. Picha na Emmanuel J. Shilatu |
|
Mgombea
pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa jimbo Ndugu Isack Mahela akiomba kura
mbele ya wajumbe 60 waliohudhuria mkutano wa uchaguzi wa jimbo la
Kigamboni. |
|
Mgombea
pekee wa nafasi ya ukatibu wa jimbo la kigamboni Ndugu Abdallah Chachala
akiomba kura mbele ya wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa jimbo la
kigamboni. Ndugu Chachala alikuwa akitetea tena nafasi yake ya ukatibu
wa jimbo la Kigamboni. |
|
Wasimamizi wa uchaguzi huo wakigawa karatasi za kupigia kura kwa wajumbe wa mkutano huo. |
|
Mjumbe wa Mkutano wa uchaguzi wa jimbo la Kigamboni kupitia Chama cha Mapinduzi, Ndugu Emmanuel John akipiga kura yake. |
|
Wajumbe wa mkutano wa uchaguzi wa jimbo la Kigamboni wakikusanya kura zao mbele ya msimamizi wa uchaguzi Ndugu Oliver Mwambope |
|
Hatimaye
matokeo yalitangawa rasmi ambapo Ndugu Isack Mahela (kushoto) alipata
kura 59 za NDIYO huku kura moja ikiharibika, na Ndugu Abdallah Chachala
(kulia) alipata zote 60 za NDIYO na hivyo kuwafanya kuwa viongozi wapya
wa jimbo la Kigamboni kupitia Chama Cha Mapinduzi. Nyuma yao ni Katibu
Mwenezi wa CCM (W) Temeke Ndugu Masunu. |
|
Katibu
mteule wa Jimbo la Kigamboni Ndugu Abdallah Chachala akitoa neno la
shukrani kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani) kwa kumchagua na
kuufanikisha salama mkutano huo wa uchaguzi. |
|
Mwenyekiti
mpya wa jimbo la Kigamboni Ndugu Isack Mahela naye pia aliwashukuru
wajumbe na kisha kuufunga rasmi mkutano wa uchaguzi wa jimbo la
Kigamboni. Wengineo wanaoonekana pichani ni viongozi wa Wilaya ambapo
kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM (W) Temeke, Ndugu Yahaya Sikunjema,
Katibu Mwenezi wa CCM, Ndugu Masunu na Mjumbe wa Kamati ya siasa (W)
Temeke, Ndugu Oliver Mwambope. Picha zote na habari Emmanuel J. Shilatu. |
0 MAOINI :