BENKI YA NMB YAMWAGA MILIONI 75 KATIKA MKUTANO WA MAKAMANDA WA POLISI MOSHI.

No comments
Tuesday, February 18, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Naibu waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Sirima akiwasili katika viwanja vya chuo cha taaluma ya polisi Moshi (MPA), mkutano mkuu wa Jeshio la Polisi mkoani Kilimanjaro, mkutano huo unadhaminiwa na NMB.
Naibu waziri wa Mambo ya ndani, Pereira Sirima (katikati, IGP Ernest Mangu kulia kwake na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro katika uzinduzi wa mkutano wa Maafisa wa Jeshi la Polisi.
Maafisa wa NMB, Meneja Mikopo Tawi la Nelson Mandela Moshi (kushoto), Saidi Pharseko na Josephine Kulwa, ambaye ni Meneja mauzo makao makuu, wakiwa katika  moja ya mabanda ya NMB katika Mkutano huo.wakipata maelezo kutoka kwa wahudumu wa banda lao.
Naibu Waziri akihutubia
Naibu Waziri katika picha ya pamoja na wadau wa Jeshi la Polisi wakiwemo wadhamini wa mkutano huo benki ya NMB.

Na Mwandishi wetu, Moshi  

BENKI ya NMB imetoa kiasi cha shilingi milioni 75, kudhamini mkutano mkuu wa siku sita wa  Maafisa wa Jeshi la Polisi nchini, ulioanza juzi katika chuo cha taaluma ya Jeshi la Polisi Moshi (MPA), mkoani Kilimanjaro.

Mkutano huo ambao unajumuisha makamishna, makamanda wa mikoa ya Tanzania bara na Visiwani pamoja na maafisa wakuu waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao makuu, ulizinguliwa na Naibu waziri wa mambo ya ndani, Pereira Ame Sirima.
Meneja wa NMB, Kanda ya Kaskazini, Vicky Bishubo (kushoto) akifaruhia  jambo na maafisa wenzake wa benki hiyo, Saidi Pharseko, Meneja Mikopo  Tawi la Nelson Mandela Moshi,Susan Shuma, meneja wateja binafsi makao  makuu na Josephine Kulwa, ambaye ni Meneja mauzo makao makuu.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja wa NMB, kanda ya Kaskazini, Bi. Vicky Bishubo, alisema udhamini huo unajumuisha usafiri wa mabasi kwa washiriki wote kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani, pamoja na maandalizi ya mkutano huo.

Alisema pamoja na hayo, NMB imetoa Kompyuta nne zitakazotumika katika mpango wa Jeshi kupambana na Uhalifu wa Mitanda,  Mikoba, Notebook na kalamu.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .