RAIS KIKWETE ALIVYOZINDUA KAMPENI YA KUPIGA VITA UUAJI WA TEMBO NA FARU KUPITIA MABANGO JUZI

Posted in
No comments
Thursday, February 13, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Rais Jakaya Kikwete (kulia) akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi  mabango hayo ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru  kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud  Mgimwa.
 Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mabango ya kuhamasisha wananchi kupiga vita mauaji ya Tembo na Faru baada ya kuyazindua rasmi kwenye  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam juzi.
Moja ya mabango hayo likiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Mahamoud Mgimwa (wa pili kushoto), akiwa na Ofisa Mteendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), Juma Pinto (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa JCTL, Juma Mabakila walipokuwa wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete kuzinduz mabango hayo.

Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, alipowasili katika hafla ya uzinduzi wa mabango hayo yatakayosambazwa sehemu mbalimbali nchini. Sehemu ya umati ulioshiriki katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mabango
JK akiwa katika hafla hiyo.
Mmiliki wa Blog ya Wananchi, William Malecela akijadiliana jambo na Juma Pinto

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .