EXCLUSIVE:MKENYA LUPITA NYONG'O ATWAA TUZO YA OSCAR

Posted in
No comments
Monday, March 3, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Kama ilivyokuwa imetarajiwa na wengi mwigizaji mashuhuri kutoka Kenya Lupita Nyong'o ambaye ni mtoto wa Waziri wa zamani nchini Kenya na Mwanasheria wa ODM, Anyang' Nyong'o, ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Oscar, kipengele cha mwigizaji bora wa kike kutokana na jukumu alilocheza la kuelezea masaibu ya Patseh katika filamu ya utumwa ya ''12 Years A Slave.''

Baada ya kupokea tuzo hilo Lupita amesema " Haikwepi mawazo yangu kwamba hata dakika moja ya furaha katika maisha yangu ni shukran na maumivu makubwa kwa mtu mwingine.''

Kisha Lupita akaongeza kusema, " Na iwe ukumbusho kwangu na kila mtoto kwamba kokote unakotoka, ndoto zako ni halisi.''

Mwigizaji Jared Leto alinyakuwa tuzo la mwigizaji bora msaidizi wa kiume kwa jukumu lake la kuelezea maisha ya mwanamke aliye na jinsia mbili aliyekuwa na akiishi na virusi vya HIV katika filamu Dallas Buyers Club.

Alilazimika kupunguza uzani kwa kipindi kifupi ili kuigiza. Sherehe ya kutolewa kwa tuzo hizo zimefanyika mjini Los Angeles nchini Marekani.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .