RC KILIMANJARO AFANYA ZIARA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJI TAKA MJINI MOSHI(MUWSA).

Posted in
No comments
Monday, March 17, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Ibrahim Msengi wakiwa na mwenyeji wao mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,(MUWSA)mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akitembelea chanzo cha maji cha Cofee Curing.
Chanzo cha Maji cha Cofee Curing.
Jengo dogo ambalo linatumika kuhifadhi dawa maalumu ya kuweka kwenye maji kwa ajili ya Chlorination.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa MUWSA.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)Injinia Cyprian Luhemeja akifafanua jambo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama wakati alipotembelea Tanki la maji la Kil.(Kulia)ni mkuu wa wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akipata maelezo kutoka kwa mafundi wa kampuni ya kuchimba visima ya DOCA inayochimba visima katika eneo la Kil Tank.
Uchimbaji wa Kisima ukiendelea.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji saf na maji taka mjini Moshi(MUWSA)Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuongoza mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, pamoja na mkuu wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi kutembelea Tanki za kuhifadhia maji eneo la CCP.
Mkurugenzi wa MUWSA ,Mhandisi Cyprian Luhemeja akimuonesha mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama eneo ambalo mamlaka hiyo inatazamia kuchimba kisima kingine kwa ajili ya kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji.
Mkuu wa mko wa Kilimanjaro Leonidas Gama akisaidiwa kuvuka wakati akitembelea chanzo kikuu cha maji cha Nsere.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Mhandisi Cyprian Luhemeja alipotembelea chanzo cha maji cha Nsere.
Afisa wa kusimamia uwekaji wa dawa katika maji,Shabani Mwamba akitoa maelezo kwa mku u wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama namna Chlorination inavyofanyika
Meneja ufundi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi, Patrick Kibasa akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama alipotembelea eneo la Mabogini kunako hifadhiwa maji taka.
Miundo mbinu ya maji taka inavyoonekana katika eneo la Mabogini.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiangalia hatua ya mwisho ya maji taka ambayo yamekuwa yakitumika kwa ajili ya umwagiliaji wa zao la Mpunga katika skimu ya Lower Moshi.
Watumishi wa mamlaka ya maji safi na maji taka wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Lleonidas Gamaalipotembelea mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa taarifa ya mamlaka hiyo kwa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama alipotembelea mamlaka hiyo kujionea vyanzo vya maji.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Ibrahim Msengi akizungumza katika kikao cha maofisa wa ngazi za juu wa MUWSA mara ya baada  ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuhitimisha zaiara ya kutembelea vyanzo vya maji.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara ya kutembelea vyanzo vya maji vya mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi (MUWSA)
Menja fedha wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,Grace Msiru akitoa neno la shukurani kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama (hayupo pichani) mara baada ya ziara ya kutembelea vyanzo vya maji vya mamlaka hiyo.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .