FABIAN JOSEPH NA JACKLINE SAKILU KIDEDEA SOKOINE MINI MARATHON 2014

Posted in
No comments
Sunday, April 13, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Polisi wilaya ya Monduli, OCD Mourice Okinda akisalimiana na baadhi ya wanariadha muda mfupi kabla ya mbio za Sokoine Mini Marathon kilomita 10 kuanza.
Waziri mwenye Dhamana na michezo, Dkt. Fenela Mukangara akianzisha mbio za Kilomita 10
Wanariadha wakichuana katika mbio za Sokoine Marathon 2014 kilomita 10 zilizofanyika jana kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine
Njia ilikuwa imejaa tope kufuatia mvua kubwa zilizonyesha
Fabian Joseph akimaliza mbio za Kilomita 10. Joseph alishinda mbio hizo
Mshindi wa pili Alphonce Felix wa Holili akimaliza mbio
Dickson Marwa wa Holili akimaliza mbio za mwaka huu. mwaka jana al;ikuwa mshindi mwaka huu kaja wa tatu
Mshindi wa mbio kilomita 10 wanawake, Javkline Sakilu akimaliza mbio hizo. Jackline Jackline Sakilu, kutoka klabu ya Winning Spirit ya  Arusha, aliibuka mshindi akitumia muda wa dakika 40:01:26,alitumia muda wa dakika
Nathalia Elisante wa Arusha akimaliza mbio katika nafasi ya pili, akitumia muada wa ambaye alitumia muda wa dakika 40:51:2.
Na Mwandishi wetu, Monduli
Mwanariadha Fabian Joseph kutoka Arusha alishinda mbio za kilomita 10  kwa upande wa Wanaume akitumia muda wa dakika 34:28.04 akimpita mwanariadha chipukizi Alphonce Felix zikiwa zimesalia kilomita moja mbio hizo zimalizike.

Nafasi ya Pili ilienda kwa, Alphonce Felix kutoka katika klabu ya  Holili, ambaye alitumia muda wa dakika 34:45.39 huku bingwa mtetezi  Dickson Marwa kutoka holili akiridhika na nafasi ya tatu akitumia muda
wa dakika 34:57.47.


Kwa upande wa mbio za wanawake, Bingwa wa mbio za Kilimanjaro marathon  kilomita 21, Jackline Sakilu, kutoka klabu ya Winning Spirit ya  Arusha, aliibuka mshindi akitumia muda wa dakika 40:01:26, huku  anafasi ya pili ikienda kwa Nathalia Elisante wa Arusha ambaye  alitumia muda wa dakika 40:51:27 na nafsi ya tatu ikashikiliwa na  Failuna Abdi, wa winning spirit, aliyekimbia kwa dakika 41:13:54.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .