KAMPUNI YA SIMU YA VODACOM YAWAUNGANISHA BUHIGWE KWENYE MTANDAO WA SIMU ZA MIKONONI
No comments
Tuesday, April 29, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiuzindua rasmi mnara wa Vodacom
kuashiria kuanza kupatikana huduma za kampuni hiyo ya simu nchini katika
kijiji cha Bukuba kilichopo Buhigwe mkoani Kigoma. Pembeni yake ni
Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine ni Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo Malcelina Mbehoma na Mwenyekiti wa
Halmashauri Abel Kabona. Vodacom inaendeleza mkakati wake wa
kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya simu za
mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma Charles Gishuli (mwenye koti)
akitumia simu yake ya mkononi kutuma fedha kupitia huduma ya M-pesa mara
tu baada ya kuzindua huduma za Vodacom katika kijiji cha Bukuba
mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum
Mwalim na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Abel Kabona. Vodacom
inaendeleza mkakati wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na
huduma za mawasiliano ya simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha
maisha yao.
Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya
Buhigwe Charles Gishuli jinsi ambavyo wakazi wa kijiji cha Bukuba Mkoani
Kigoma wanavyoweza kupata huduma za Intaneti kupitia mtandao wa Vodacom
mara baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua rasmi huduma za Vodacom
kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kushoto (mwenye kofia nyekundu) ni
Mhandisi wa Vodacom Mkoa wa Kigoma Adam Nyamgali.
Mkuu
wa Wilaya ya Buhigwe Charles Gishuli akiongea na wakazi wa kijiji cha
Bukuba na vijiji jirani waliofika kushuhudia uzinduzi wa mnara wa
mtandao wa Vodacom kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Kulia ni Meneja
Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Wengine kutoka kuhsoto ni
Mhandisi wa Vodacom Adam Nyamgali, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Renatus
Mkasa na Kaimu Mkurgenzi Mtendaji wa Wilaya Malcelina Mbehoma.
Kupatikana kwa huduma za Vodacom kijijini hapo kunatarajiwa kufungua
ukurusa mpya wa maendeleo ya kiuchumi an kijamii kijijini hapo.
Mhandisi
wa Vodacom Mkoani Kigoma Adam Nyamgali akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya
Buhigwe Mkoani Kigoma jenereta inayozalisha umeme wa kuendeshea mnara wa
mawasiliano wa kampuni hiyo. Mkuu huyo wa Wiayaa aliuzindua mnara huo
uliopo kijiji cha Bukuba mwishoni mwa wiki. Vodacom inaendeleza mkakati
wake wa kuwaunganisha watanzania wa vijijini na huduma za mawasiliano ya
simu za mkononi ili kuwawezesha kuboresha maisha yao.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :