KUELEKEA MCHEZO WA LEO: MBEYA CITY FC YATOA ONYO KWA AZAM FC
No comments
Sunday, April 13, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kwanza nachukua
nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wapenzi wote wa mchezo wa mpira wa miguu na
wapenzi wa Mbeya City Fc popote pale walipo kwa kuiunga mkono timu yao muda
wote wa michezo ya ligi kuu inayoelekea ukingoni hivi sasa.Klabu inathamini
nafasi ya wapenzi na washabiki katika kujenga timu imara na yenye ushindani
kama walivyofanya kwa timu yetu.
Timu yetu ilianza
ligi msimu huu 2013/2014 ikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa au kuwa katika
nafasi za juu za ligi yetu.Hiyo ndiyo dhamila iliyokuwepo kwa
viongozi,wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Michezo miwili
imesalia kwa timu yetu kabla ligi kuu ya Vodacom kumalizika katika msimu huu
2013/2014.katika safari yetu ya ligi kuu kwa mara ya kwanza msimu huu, changamoto
nyingi za kiutawala na za kimtazamo kutoka kwa wadau wote wanaohusika na mchezo
wa mpira wa miguu nchini tumezishuhudia .
Changamoto hizo ni
ikiwemo upangaji wa ratiba usiyokuwa na uwiano mzuri,baadhi ya mechi kuamuliwa
vibaya na waamuzi wa mchezo,wizi wa mapato ya milangoni unaotokana na mfumo
mbaya wa uuzaji wa tiketi,uadilifu mdogo kwa baadhi ya viongozi wenye dhamana
ya kusimamia mpira katika ngazi zote n,k.
Kuelekea mchezo
wetu wa tarehe 13/04/2014 dhidi ya AZAM FC kumezuka propaganda chafu na ambazo
si sahihi katika ukuzaji wa mpira hasa wa ligi ndogo kama ya Tanzania. Nachukua
nafasi hii kutoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo ambayo yamekuwa sehemu ya
propaganda hizo:
1. Klabu
imehaidiwa kununuliwa basi na hivyo inajiandaa kutoa ushindi kwa kwa timu ya
AZAM Fc na kuwarahisishia mazingira ya Ubingwa.
Halmashauri ya
jiji la Mbeya limekuwa katika mchakato wa kutafuta na kununua basi kwa ajili ya
matumizi mbalimbali ya Halmashauri ikiwemo kutumiwa na timu zake (
Netiboli na Mpira wa miguu)ambazo zote zipo ligi kuu ya michezo husika kwa
kufuata sheria ya manunuzi ya Umma. Mchakato huo ulianza tarehe 8/8/2013 halmashauri
ilipotangaza nia hiyo katika gazeti la “the guardian” la tarehe
hiyo kwa tender no.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01 hii
ni baada ya Halmashauri kutenga bajeti ya fedha za makusanyo yake ya
ndani kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na 2013/2014 ili kukidhi haja hiyo.
Tangazo hilo
halikupata mzabuni mwenye sifa za kufanya usambazaji wa basi hilo hivyo tangazo
hilo lilirudiwa tena tarehe 12/2/2014 katika gazeti la majira kwa Tender No.LGA/069/2013-2014/MCC/G/01
(Re-advitised), Mchakato na maandalizi ya ufunguaji wa ufanyaji
wa tathmini wa zabuni hiyo unaendelea kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya Umma.
Pamoja na mchakato
huo hapo juu,pia klabu inaendelea na mazungumzo na wadau mbalimbali wenye nia
ya kuwekeza kwa udhamini wa bidhaa zao,moja ya maeneo ya udhamini ni pamoja na
ununuzi wa basi la wachezaji taratibu na makubaliano haya yatakapo kamili
umma wa wapenda mchezo wa mpira wa mguu utajulishwa.
Hivyo propaganda
hiyo kuwa klabu imehongwa basi si za kweli na si sahii ila zina nia ya
kuidhalilisha timu yetu.
2. Propaganda
kuwa Mwalimu Juma Mwambusi kanunuliwa nyumba Maeneo ya chamazi ili apange
kikosi dhaifu siku ya mchezo tarehe 13/4/2014.
Mwalimu(Kocha)
Juma Mwambusi ni muajiliwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya,kwa maana hiyo ni
mtumishi wa Umma. Mwalimu Mwambusi amekuwa na timu yetu kwa muda mrefu sasa na
ataendelea kuwepo.Kumekuwepo na maneno yasiyofaa dhidi ya mwalimu wetu toka
mzunguko wa pili wa ligi kuanza,maneno haya yamekuwa na nia ya kuaribu muenendo
wa timu ili ianze kufanya vibaya lakini zaidi ya hapa yana nia ya kumdhalilisha
mwalimu wetu na taaluma ya ukocha nchini.
Mwalimu
amefedheheshwa sana na taarifa hizo.
3. Propaganda
kuwa wachezaji wote wa kikosi cha kwanza wamepewa hongo wacheze chini ya
kiwango 13/4/2014.
Wachezaji ndiyo
wachezaji wenye nidhamu kubwa katika ligi ya mwaka huu ndani na nje ya uwanja
muda wote,ni waadirifu na wanajua wanataka nini.Mpira ndiyo ajira yao kama
watumishi wa umma ndani ya Halmashauri ya jiji la Mbeya.Hawajawahi na wala
hawatawahi kuchukua rushwa kwa lengo la kupanga matokeo.
Klabu yetu
haisadiki katika upangaji wa matokeo ya mchezo wa mpira wa miguu kwani tunajua
fika kuwa hakutaisadia kama klabu lakini pia kama taifa katika kuendeleza mpira
wa miguu nchini.
Hitimisho,
Mchezo wa mpira wa
miguu una matokeo matatu kushinda,kushindwa na kutoka sare. Klabu inaamini kuwa
timu iliyojiandaa vizuri kama yetu inastahili kupata matokeo mazuri uwanjani.Falsafa
mojawapo ya timu yetu ni kushinda mechi kwa kucheza mpira unaovutia na
kuwaburudisha watazamaji.
Tuhuma mbalimbali
za upangaji matokeo katika ligi yetu zimeanza kuota mizizi hasa ligi inapoingia
mzunguko wa pili ,katika suala hili kama ambavyo linataka kuhusishwa nasi
yawezekana propaganda hizi kwa upande wa timu inayotuhumiwa kuandaa michakato
hiyo wana uzoefu nalo na yumkini ndiyo chachu ya mafanikio yao mpaka kufikia
hatua hiyo waliofikia sasa.
Kama timu hiyo
inauwezo wa kirasilimali wa kufanya uovu huo wote iweje ishindwe kuwa na timu
imara na ya ushindaji mpaka itegemee kutafuta wachezaji wa timu pinzani kupata
matokeo mazuri?
Timu yetu ndiyo
timu pekee changa miongoni mwa timu tano zinazoongoza msimamo wa ligi yetu kwa
sasa,si hivyo tu bali ndiyo timu pekee inayoundwa na wachezaji wengi wapya
katika ulimwegu wa soka na inayoundwa na Watanzania watupu kuanzia
wachezaji,benchi la ufundi pamoja na viongozi.Hii inathibisha kuwa kama taifa
tunaweza kufanya kazi nzuri bila kutegemea wachezaji toka nje baadhi yao
wasiokuwa na tija.
Mpira ni ajira
hatuna budi kuuratibu vema ili kutoa nafasi inayostahili kwa vijana wetu ili
kupunguza tatizola ajira nchini lakini pia kutumia vipaji vyao kulipa taifa
muonekano stahili.
Mamlaka
zinazohusika hazina budi kuanza kufuatilia na kuchukua hatua kali kwa baadhi ya
timu zinzohusishwa na upangaji wa matokeo ili kulinda heshima ya mchezo huo
bila kuogopa uwezo wa rasilimali wa timu hizo.
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
9.04.2014
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :