MADAKTARI WAKUZA UKE KATIKA MAABARA KWA MARA YA KWANZA
Posted in
Afya
,
Teknolojia
No comments
Wednesday, April 16, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Madaktari nchini Marekani wamefanikiwa kuwatengezea wanawake wanne sehemu ya uke kwa njia ya kisayansi.Ni mara ya kwanza kwa uke wa mwanamke kukuzwa katika maabar.
Wataalamu walisema kuwa utafiti wao, ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la kisayansi la Lancet, ni mfano wa hivi karibuni wa nguvu za mbinu tofauti na za kisasa za matibabu.Wanawake hao walizaliwa na uke ambao haukuwa umeumbika vyema yaani ulikuwa na kasoro ya maumbile , tatizo linalojulikana kama ‘vaginal aplasia.’
Matibabu ya kisasa kwa tatizo kama hilo la kiafya yanaweza kuhusisha upasuaji ambapo ngozi au sehemu ya utumbo inatumika.Celi zilichukuliwa kutoka kwa kizazi cha kila wanawake hao ambacho kilikuwa na kasoro ya maumbile na kukuzwa katika maabara ili kuweza kuzaana.
Picha za kizazi cha wanawake hao zilitumiwa kuwarekebishia uke wao.Hili bila shaka ni jambo geni katika sayansi ya matibabu na pia inatoa taswira ya mambo yatakavyokuwa katika siku za usoni.
Jambo la Kutumia celi za mwili kubadilisha maisha ya wagonjwa tayari limefanyika na kuwasiaidia wagonjwa kupata kibofu cha mkojo, mishipa ya damu na koo. Sasa katika orodha hiyo unaweza kuongeza kwenye uke na pua.
Habari Zingine
- Je Wajua Samaki Wabichi ni Dawa?
- Cheki viatu vinavyotumia bluetooth kukuelekeza popote uendako
- Hizi ndio Treni mbili za kifahari zinazotengenezwa, nchini Japan, kuanza kutumika May 2017
- Simu ya Roboti yaziduliwa leo
- Uswisi kuzindua Reli ndefu zaidi Duniani inayopita 'underground' imejengwa kwa miaka 17
- China yatengeneza mabasi yanayopita juu ya magari mengine (tizama Video)
- Fahamu nchi zinaongoza kwa matumizi ya Bangi
- Kuwa na mpenzi na afya nzuri huchangia furaha
- Mji wa Dodoma, nchini Tanzania yakumbwa na ugonjwa usiojulikana
- Tanzania kinara unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :