PINDA MGENI RASMI, HAFLA YA KUKABIDHI HUNDI ZA RUZUKU KWA WACHIMBAJI WADOGO.
Posted in
Matukio
No comments
Tuesday, April 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
|
|||
|
|
|
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda atakuwa mgeni rasmi katika
hafla iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini ya kukabidhi hundi za ruzuku
ya Dola za Marekani 500,000 kwa wachimbaji wadogo 11 waliokidhi vigezo.
Hafla ya Utoaji wa hundi
hizo kwa wachimbaji wadogo itafanyika mjini Dodoma tarehe 9/4/2014 katika Chuo
cha Madini ambapo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
akiambatana na Naibu Waziri
anayeshughulikia Madini, Stephen Masele pamoja na watendaji kutoka Benki ya
Rasilimali Tanzania (TIB), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na
Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA) watashuhudia utoaji wa hundi
hizo.
Ruzuku hiyo ya Dola za Marekani 500,000 imetolewa
na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP)
ulio chini ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kutolewa kwa hundi hizo ni
matokeo ya mkataba ambao Wizara ya Nishati na Madini iliingia na Benki ya
Rasilimali Tanzania (TIB) ili Benki hiyo iwe Wakala wa kutoa mikopo na ruzuku
kwa wachimbaji wadogo kwa niaba ya serikali.
Mkataba wa uendelezaji
wachimbaji wadogo ulioingiwa kati ya TIB na Serikali unasisitiza ruzuku
kutolewa kwa wachimbaji wadogo wenye sifa ili kuwawezesha kufanya shughuli zao
za uzalishaji mali, wakiwepo wanawake wanaojishughulisha na utoaji huduma
katika maeneo ya uchimbaji mdogo.
Wachimbaji wadogo 11
watakabidhiwa hundi hizo za ruzuku baada ya kukidhi vigezo vya kuwa na uzoefu
wa uchimbaji mdogo usiupungua miaka Tano, kuwa na leseni hai ya uchimbaji,
uchenjuaji na biashara ya madini pamoja na kuwa na ushahidi wa upatikanaji wa
mashapo au mali ghafi inayohitajika kwa ajili ya mradi unaoombewa ruzuku.
Imetolewa na;
BADRA MASOUD
MSEMAJI WA WIZARA
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :