KIDEFU WATOA MIL. MOJA KWA ATAKAYEFANIKISHA KUKAMATWA WEZI WA LAMI
Posted in
Jicho la Habari
No comments
Tuesday, May 6, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
wajumbe wa mkutano mkuu wa mfuko wa maendeleo ya wananchi wa Tarafa ya Kibosho wakinsikiliza mwenyekiti wao(hayupo pichani),Morris makoi katika mkutano uliofanyika jumatatu wiki hii huko kibosho. |
Mwandishi wetu, Moshi
MFUKO wa maendeleo wa wananchi wa Tarafa ya Kibosho wilaya ya Moshi Vijijini,umetoa ahadi ya zawadi ya pesa taslimu shilingi Milioni moja kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa watu waliohusika na tukio la wizi wa lami mali ya mfuko huo.
Ahadi hiyo ilitolewa jana na mwenyekiti wa mfuko huo, Morris Makoi katika mkutano mkuu maalumu wa wanachama wa mfuko huo kufuatia wizi wa mapipa 35 uliofanywa na watu wasiojulikana Apili 17 mwaka huu.
Lami hiyo ambayo imedumu kwa maiaka 17 sasa,imekuwa haina uangalizi mzuri kutokana na kukosekana kwa ulinzi wa uhakika na kutoa mwanya kwa wezi kuiba kiurahisi bila kukamatwa.
Akizungumza katika mkutano huo ambao hata hivyo uliahirishwa kutokana na kutofia idadi stahiki ya wajumbe,Makoi alisema kuwa,mtu yeyote mwenye taarifa sahihi juu ya nani aliiba lami hiyo na wapi imeuzwa,awasiliane na uongozi wa KIDEFU .
Mfuko huo wa maendeleo ya wananchi wa tarafa ya Kibosho ulianzishwa kwa lengo la kuharakisha maendeleo kwa wananchi ikiwamo ujenzi wa shule,hospital na kuboresha miundombinu ya barabara .
Katika kufanikisha mfuko huo,wananchi walikuwa wakikatwa shilingi mbili kwa kila kilo moja ya kahawa kwa ajli ya kutunisha mfuko huo na lami hiyo ilikuwa itumike kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Hata hivyo mfuko huo uliyumba na kusambaratika na hivyo kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa ambako kwa sasa wananchi wameamua kwa makusudi kuufufua mfuko huo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti makoi ambaye pia ni diwani wa kata ya Okaoni na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Moshi,wizi huo unatokea kutokana na kutokuwapo na usimamizi mzuri wa mali za mfuko huo kwa miaka kumi sasa..
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :