Showing posts with label Jicho la Habari. Show all posts
Showing posts with label Jicho la Habari. Show all posts

Nawaza kwa Sauti: Leo Nimemkumbuka Shujaa Patrice Lumumba

Nawaza kwa Sauti: Leo Nimemkumbuka Shujaa Patrice Lumumba

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Leo nimemkumbuka sana shujaa wa nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Patrice Lumumba, nikaamua kuirudia kuisoma barua yake aliyomwandikia mke wake Pauline na watoto wake muda mchache kabla hajauwawa mwaka 1960.

Ni barua ambayo siku ya kwanza nilipoisoma miaka kadhaa huko nyuma ilinitoa machozi sana. Katika barua ile alimwambia mke na watoto wake kuwa hana uhakika kama barua ile itawafikia lakini pia hana uhakika kama ataweza kuwaona tena.

Juu ya yote alieleza kuwa anajisikia fahari sana kwa kuwa hayuko tayari kuwa kibaraka wa kikoloni na kuwasaliti wananchi wa kongo kwa jambo lolote lile,yuko tayari kufa ili mradi anasimamia jambo sahihi kwa manufaa ya wengi. Barua hii inanikumbusha maneno ya Emiliono Zambata,kamanda wa jeshi na mwanamapinduzi wa mexico aliyesema:

”Ni bora kufa umesimama kuliko kuishi huku umepiga magoti”.Ghafla nikakumbuka maneno ya mwanaharakati mweusi wa marekani, Martin Luther Jr aliposema-“Kama haujapata jambo ambalo uko tayari kutoa uhai wako kwa hilo basi haufai kuendelea kuishi”,maneno haya makali yakanipeleka kwa Steven Bikko aliyesema-“Ni bora kufa kwa wazo litakaloishi kuliko kuishi kwa wazo litakalokufa”

Watu hawa hawakumaanisha kuwa hawapendi kuishi na wanapenda kufa hovyohovyo,la hasha.Walimaanisha kuwa kwenye maisha yao wamepata sababu zenye nguvu na msingi zaidi kuliko kuishi ili kula, kunywa, kununua gari, kuoaau kuolewa na kuwa na watoto. Wanamaanisha kuwa kama unataka kuwa mtu unayeleta tofauti katika kizazi chako ni lazima uwe mtu uliye tayari kujitoa kwa ajili ya wengine.Siku moja mwaka 2002 wakati nasoma biblia nilikutana na ujumbe wa Mwanzo 45:5,”


..Yusufu akawaambia kaka zake,Ingawa ninyi mliniuza ila Mungu alikusudia Kunitanguliza ili niwasaidie(To save your life)”Nikasikia ujumbe ndani yangu-“Nawe umetumwa ili uwasaidie wengine”.Kuanzia hapo nilianza kujifunza mambo mengi sana na kujaribu kufanya kila nililoweza kwa ajili ya kuchangia mafanikio ya wengine.

Mabadiliko katika nchi yoyote yanaletwa pale kunapokuwepo na watu walio tayari kuishi maisha ya kujito, najua unasoma ujumbe huu kwa sababu wewe ni mmoja wao.Kumbuka kile Mama Theresa Alichosema-“Hakuna anayeweza kuwasaidia watu wote,lakini kila mtu anaweza kumsaidia angalau mtu mmoja”


Watu wanaoleta mabadiliko katika kizazi chao ni watu ambao wanaamini kuwa wanao wajibu mkubwa kwa jamii yao bila kujali nafasi waliyonayo kwa sasa.Angalia kile ambacho unatamani kibadilike na chukua hatua ya kubadilisha.


Safari ya kuchangia mabadiliko katika jamii na nchi yako yanahitaji uvumilivu sana,usikubali kukata tamaa kwa sababu ulifanya kitu hakikuwa na matokeo.Katika nchi nyingi watu wanaosimamia haki na mabadiliko ya dhati huchukiwa na watu wabaya wako tayari kuwaondoa duniani.

Tunahitaji kizazi kipya cha watu ambao si wale walio tayari kumwaga damu za wengine ili wao wabakie katika nafasi bali wale walio tayari kutoa uhai wao ili kuokoa uhai wa wengine.Wako wapi akina Mandela wa leo ambao hawakusukumwa na cheo bali walisukumwa na ukombozi wa mtu mweusi.


Wako wapi akina Nyerere wa leo ambao hawakusukumwa na kutafuta umaarufu na utajiri kupitia nafasi zao bali walisukumwa na uzalendo na upendo kwa nchi yao,ambaye hadi anakaribia kukata roho bado anasema-“Najua Watanzania watanililia,lakini nitawaombea kwa Mungu”

Ile sauti najua haikuwa ya peke yangu,najua nawe unaisikia ndani yako,najua kipo kizazi kipya kinachoamini katika kujitoa kwa ajili ya jamii na nchi yao sio kwa ajili ya faida yao wenyewe bali kwa ajili ya faida ya wengine na kizazi kijacho.

Patrice Lumumba ambaye hata mifupa yake iliyeyushwa kwa tindikali ili kufuta ushahidi ,sauti yake bado inalia kutoka katika misitu ya kongo kwenda kila nchi ya bara la Afrika-Inalia na kuita "Wako wapi Vijana wa kizazi cha leo walio tayari kujitoa kwa nchi yao?” Nawaza kwa Sauti



Shukran: Joel Arthur Nanauka

Katibu Mkuu amuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini

Katibu Mkuu amuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza mbele ya Mabalozi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Sinikka Antila. Katika hotuba yake Balozi Mulamula alimshukuru Balozi Antila kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Finland. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza.
Balozi Antila (Wa kwanza Kulia), Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (Wa pili Kutoka kulia), Balozi wa Uingereza Mhe. Dianna Melrose (Wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Segore Kayihura (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Egon Kochanke (Wa pili kutoka kulia) na Balozi wa Canada nchini Mhe. Alexandre Leveque wakimsikiliza Balozi Mulamula hayupo pichani 
Sehemu ya Wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani).
Balozi Antila akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo aliishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo nchini.
Katibu Mkuu Mhe. Balozi Mulamula (Wa kwanza kushoto) kwa pamoja na, Mkurugenzi Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine (Wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregond (Wa pili kutoka kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bwa. Alvaro Rodriguez  wakimsikiliza Balozi Antila (hayupo pichani).
Balozi Antila akiendelea Kuzungumza
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakitakiana afya njema kwa kugonganisha Glasi
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza.
Balozi Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlango wa Zenji Balozi Antila. Chanzo: michuzi blog

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAIFA LA SWEDEN

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAIFA LA SWEDEN

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
 Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
 Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye kilemba).
 Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani) Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha Hemela akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WAFANYA MKUTANO MKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM KUJAILI MCHANGO WA DIPLOMASIA KATIKA KUFIKIA DIRA YA TAIFA 2025

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WAFANYA MKUTANO MKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM KUJAILI MCHANGO WA DIPLOMASIA KATIKA KUFIKIA DIRA YA TAIFA 2025

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania ulioanza Mei 25-27, 2015 katika hoteli ya Ramada, Dar es Salaam. Lengo kuu la mkutano huo ni kujadili utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje na mchango wa Wizara kufikia Dira ya Taifa 2025. Mkutano huu ni wa nne kufanyika tangu ule wa kwanza uolifanyika mwaka 1999 katika hoteli ya Whitesands, Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya mkutano ni Diplomasia ya Tanzania Kuelekea Dira ya Taifa 2025. Ujumbe huo umechaguliwa kwa kuzingatia mchango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika juhudi za kutimiza ndoto ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wa pili kutoka kushoto) akiongea wakati wa Mkutano wa Mabalozi wa Tanzania  ulioanza Mei 25-27, 2015 katika hoteli ya Ramada, Dar es Salaam.

Kutoka kulia ni Balozi Liberata Rutageruka Mulamula ambaye ameziwakilisha nchi za Marekani na Mexico ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi ambaye anawakilisha nchi za India,  Sri Lanka, Singapore na Nepal.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa Balozi Yahya Simba akitoa shukrani kwa viongozi waliweza kufanikisha mkutano huo.
Mabalozi wanaowakilisha Tanzania Nchi za Nje kutoka nchi mbali mbali wanaohudhuria mkutano huo.
Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbali mbali wanaohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini.

Africa Day 2015 is an opportunity to celebrate the development of the African continent as well as consider the various opportunities that it offers - DHL

Africa Day 2015 is an opportunity to celebrate the development of the African continent as well as consider the various opportunities that it offers - DHL

No comments
By danielmjema.blogspot.com
CAPE-TOWN, South-Africa, May 25, 2015/ -- Africa Day 2015 is an opportunity to celebrate the development of the African continent as well as consider the various opportunities that it offers. This is according to Charles Brewer, Managing Director of DHL Express Sub-Saharan Africa (SSA) (http://www.dpdhl.com), who not only believes that the continent offers vast opportunities but also that it is one of the last frontiers for economic growth and development.




Photo Charles Brewer: http://www.photos.apo-opa.com/plog-content/images/apo/photos/charles-brewer-1.jpg (Charles Brewer, Managing Director for DHL Express Sub-Saharan Africa)

Africa Day is the annual commemoration of the founding of the Africa Union (AU), and acts as a reminder of the continent’s rich culture, diversity as well as its resilience and the various developing economies on the continent.

Brewer explains that as DHL Express has been present in Africa for 37 years, the company has witnessed the turnaround from the ‘forgotten continent’ to ‘Africa Rising’, which has been an amazing and insightful experience.

“Despite the recent prediction by the World Bank  that economic growth in Sub-Saharan Africa will slow in 2015, the continent still remains relatively unexplored which indicates untapped opportunities in the region. We remain positive about Africa’s potential and believe that it’s time for the continent to focus on the opportunities, connect across the continent to leverage cross-border and global opportunities and grow as one.”

To meet the increased needs of the burgeoning middle class in the region, DHL Express has continued their aggressive expansion strategy in their efforts to make logistics more accessible. “With the rise of e-commerce, global markets are more attractive and accessible to individuals and local businesses, therefore we need to make sure that we are well positioned to cater to their needs. We currently have 3800 retail outlets across Sub Saharan Africa,” adds Brewer.

In the spirit of Africa Day, Brewer also points to one of the many projects conceptualised and implemented by DHL Express on the continent – DHL Africa as One - which highlights the company’s continuous commitment to investing in Africa. “As part of this epic journey, a team from DHL, the official logistics partner of Rugby World Cup 2015, is driving across Africa in three Land Rover Discoveries, while capturing every step of the journey, every person, every place and every pass on film, in photographs and words, and then sharing this content with Africa and the world. Part of the journey includes passing a single rugby ball from hand to hand through 45 African countries, over 11 months, from Cape Town and ending in London in September 2015.

We have passed the half way mark and the team is currently in Niger, en route to Chad. The tour is not just about rugby, but about showcasing Africa to the rest of the world and making an impact on the continent. In addition to the rugby clinics that take place as part of the journey, we are distributing over 500 000 units of stationery to young children and providing free eye tests for thousands of people, through our partnership with Mercy Ships.”

More than ever, global companies are now looking to expand into Africa and invest in its diverse markets and people. “DHL is committed to play a continued role in developing the continent through its investments and initiatives aimed at connecting Africa to the world,” concludes Brewer.
 

Tanzanian Mayunga Malimi is the winner of Airtel TRACE Music Star grand finale

Tanzanian Mayunga Malimi is the winner of Airtel TRACE Music Star grand finale

No comments
By danielmjema.blogspot.com

 You chose Mayunga Nalimi! Tanzania's contestant seduced you and the judges Akon, Lynnsha and Devyne Stephens. After a finale full of unexpected developments, Mayunga has been one of the only to keep his calm during his performances. That's probably why he fainted just after he heard final verdict!

Mayunga Malimi has quickly attracted judges' eyes with great live and acapella performances. He also took advantage of Laurna and Jitey failures in the last round of the finale to take the title back home. He will now join Akon in the studio to work on his first single. A new superstar is born!

Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) Pt I

Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) Pt I

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo Nani alimfanya ashawishike na fani hii? Maisha yake kimahusiano je? Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake? KARIBU.

Katika kipindi cha "HUYU NA YULE" leo, usikose kujua UNDANI wa maisha ya Linda

Katika kipindi cha "HUYU NA YULE" leo, usikose kujua UNDANI wa maisha ya Linda

No comments
By danielmjema.blogspot.com
NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Leo Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda

Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho

MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO.

MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO.

No comments
By danielmjema.blogspot.com
 Watoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.
 Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.
 Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.
 Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA WASABATO WAISHIO NCHINI MAREKANI

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA MKUTANO MKUU WA WASABATO WAISHIO NCHINI MAREKANI

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.
Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake  Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.  
Nchungaji Herry Mhando akifanya mamombi maalum kabla ya kumkaribisha mchungaji Wilbert Nfubhusa kutoa mahubiri,
Mshereheshaji Magoma akifafanua jambo
Mhahubiri yakiendelea
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

TBN YAMUOMBA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ASIPITISHE MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015

TBN YAMUOMBA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ASIPITISHE MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015

No comments
By danielmjema.blogspot.com
TAARIFA KWA UMMA YA TBN

KUMUOMBA MH. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE ASIPITISHE
MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015

Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni. 

Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015
Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika.

Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea habari.

Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu.

Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho wa sahihi?

Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari.

Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu kihisia.

Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013.

Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’

Hii iki maanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa habari nchini.

Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika

IMETOLEWA NA;
Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network-TBN)
04/03/2015.

SKYLIGHT BAND INAKUKARIBISHA LEO THAI VILLAGE KABLA YA KUELEKEA JIJINI ARUSHA JUMAPILI HII

SKYLIGHT BAND INAKUKARIBISHA LEO THAI VILLAGE KABLA YA KUELEKEA JIJINI ARUSHA JUMAPILI HII

No comments
By danielmjema.blogspot.com



IMG-20150402-WA0076
John Music (katikati) akitoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita huku akipewa sapoti ya Back vocal na Ashura Kitenge (kushoto) pamoja na Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 (kulia)
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47(katikati) akiimba na wenzake ambao ni Sam Mapenzi(kulia) pamoja na Ashura Kitenge (kushoto)
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kubwa mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani) kwenye kiota cha Thai Village, Masaki jijini Dar
Waimbaji wa Skylight Band wakisakata rhumba
John Music (katikati) akitoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar

Waimbaji wa Skylight Band wakiimba kwa pamoja moja ya nyimbo za bendi yao
Mwimbaji wa Skylight Band Sony Masamba akiimba na kucheza pamoja na Aneth Kushaba AK 47(kulia) pamoja na Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower(kushoto)
Hapa ilikuwa ni kusugua mpaka utakate tu, njoo leo ujifunze style ya kusugua mpaka ujue.
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani mbele ya mashabiki wao(hawapo pichani)
Ni mwendo wa Bolingo tu mpaka kuchweee
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akitoa burudani kwa hisia kali ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar
Binti mrembo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni Ashura Kitenge akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band (hawapo pichani) huku akipewa sapoti na Sam Mapenzi katika show yao ya Ijumaa iliyopita ndani ya koita cha Thai Village-Masaki.  
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (katikati) na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
DSC_0251

Sugua sugua mpaka utakate ni nomaaaama saaanaa karibu leo kuna mambo  mazuri ndani ya Skylight Band

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .