KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NJE AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA TAIFA LA SWEDEN
Posted in
International
,
Jicho la Habari
No comments
Wednesday, June 10, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Mgeni
rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula
akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa
Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
Balozi
wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla
hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi
huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Filberto Cerian Sebregondi
akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Liberata
Mulamula huku Afisa wa Wizara hiyo Bi.Asha Mkuja (kushoto mwenye
kilemba).
Mkuu
wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe.Balozi Juma Halifan
Mpango akisalimiana na Balozi Liberata Mulamula.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Balozi Mulamula (hayupo pichani) Afisa wa wizara ya Mambo ya Nje Bi.Asha Hemela akifuatilia hotuba ya mgeni rasmi katika hafla hiyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :