By
danielmjema.blogspot.com
|
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi
Libarata Mulamula akizungumza mbele ya Mabalozi na Wageni waalikwa
wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa
ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi
nchini, Mhe. Sinikka Antila. Katika hotuba yake Balozi Mulamula
alimshukuru Balozi Antila kwa mchango wake wa kuimarisha ushirikiano
kati ya Tanzania na Finland. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya
Serena Jijini Dar es Salaam. |
|
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza. |
|
Balozi
Antila (Wa kwanza Kulia), Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi
Juma Mpango (Wa pili Kutoka kulia), Balozi wa Uingereza Mhe. Dianna
Melrose (Wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene
Segore Kayihura (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini
Mhe. Egon Kochanke (Wa pili kutoka kulia) na Balozi wa Canada nchini
Mhe. Alexandre Leveque wakimsikiliza Balozi Mulamula hayupo pichani |
|
Sehemu ya Wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani). |
|
Balozi
Antila akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo aliishukuru Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Serikali kwa ujumla kwa
ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo nchini. |
|
Katibu
Mkuu Mhe. Balozi Mulamula (Wa kwanza kushoto) kwa pamoja na, Mkurugenzi
Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine (Wa pili kutoka
kushoto), Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregond (Wa pili
kutoka kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
Bwa. Alvaro Rodriguez wakimsikiliza Balozi Antila (hayupo pichani). |
|
Balozi Antila akiendelea Kuzungumza |
|
Balozi Mulamula na Balozi Antila wakitakiana afya njema kwa kugonganisha Glasi |
|
Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga
ambaye alikuwa mshereheshaji wakati wa hafla hiyo akizungumza. |
|
Balozi Mulamula akimkabidhi zawadi ya picha ya Mlango wa Zenji Balozi Antila. Chanzo: michuzi blog |
0 MAOINI :