MTAALAMU WA NYASI BANDIA KUTOKA FIFA DR.IAN McCLEMENTS ATUA BUKOBA, APIMA UWANJA WA KAITABA LEO
Posted in
Michezo
No comments
Monday, May 5, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mtaalamu
wa nyasi bandia kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA), Ian McClements amewasili Bukoba leo hii Asubuhi kwa Ndege ya
kukodi. McClements
akiwa hapa Bukoba amekagua Uwanja wa Kaitaba, na baadae amekwea tena
ndege yake kuelekea jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Viwanja
hivi vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa
misaada wa Goal Projects. Baada ya ukaguzi huo, McClements atatuma
ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liweze kuteua mkandarasi wa kufanya
kazi hiyo.
Kwa
Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal
Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar
es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
Dr. Ian McClements (kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Eng. George Geofrey wa Manispaa hapa Bukoba
Dr.
Ian McClements akichimba chini ili kupima na kuona udogo upi ulipo
chini, Amehimba katika maeneo matatu tofauti tofauti na kubaini tofauti.
Ili chukua muda wa dakika 1 na sekunde 40 tu maji yalikuwa yameishatoweka
Akipima maji aliyoweka
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :