PANONE FC YAPANDA DARAJA; YAICHAPA SMALL TOWN.
Posted in
Michezo
No comments
Tuesday, June 3, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
KIKOSI CHA TIMU YA PANONE FC WAKIWA KATIKA PICHA KABLA MCHEZO WAO
Panone FC kutoka Kilimanjaro imefanikiwa kupanda daraja la kwanza, baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa mwisho.
Panone ambayo ilikua katika kituo cha Mbeya, ilikuwa ikichuana kuwa kati ya vilabu vitatu vitakavyopanda daraja kutoka katika vituo vitatu vya Mbeya, Shinyanga na Morogoro.
Katika Kituo cha Mbeya kulikua na Takribani timu Tisa kutoka katika Mikoa Tisa ya Tanzania Bara ambapo Moja ya Mkoa uliopangiwa katika kituo hicho ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro uliowakilishwa na Timu ya Panone Fc.
Timu ya Panone Fc iliweza kushuka Dimbani hapo jana katika mchezo wao wa Mwisho Dhidi ya Timu ya Small Town ya Ruvuma ambapo mchezo huo ulipigwa saa Kumi kamili katika uwanja wa Vwawa wilaya ya Mbozi. Katika mchezo huo Timu ya Panone Fc ilihitaji Ushindi ili iweze kufuzu mashindano Huku nayo timu ya Njombe Mji ya Mkoa wa Njombe ikiwa inachuana na Timu ya AFC ya Arusha katika uwanja wa Mbeya Mjini huku Njombe wakiwa wanahitaji Ushindi na kuiombea Panone Fc ipoteze mchezo ili iweze Kushinda.
Katika Mchezo wa Jana Hali ilikua tofauti mnamo wa Dakika ya Tatu Mchezaji wa Panone Fc Ramadhan Hasan Aliweza kuiandikia Goli la Kwanza Timu yake na kuamsha Mashambulizi na Hari mpaka Dakika ya Sita ya Kipindi cha kwanza ndipo Ayoub Ruben alipoifungia Goli la Pili Timu ya Panone Fc na kuyazima matumaini ya Timu ya Small Town ya Ruvuma. Mpaka Mpra kuisha Panone Fc ilipata ushindi wa Goli mbili kwa bila dhidi ya Small Town ya Ruvuma huku Timu ya Njombe Mji na AFC ikitoka Sare ya Goi moja kwa moja na Matokeo hayo yakazima ndoto za Timu ya Njombe mji huku Nyota ya Panone Fc iking'ara.
Kutokana na Ushindi huo Timu ya Panone Fc imeweza kupanda Daraja na kwenda Daraja la kwanza na kuufanya mkoa wa Kilimanjaro kupata Timu ambayo itashiriki Ligi Daraja la kwanza ambayo waliikosa kwa kipindi kirefu.
Timu ya Panone Fc iliweza kushuka Dimbani hapo jana katika mchezo wao wa Mwisho Dhidi ya Timu ya Small Town ya Ruvuma ambapo mchezo huo ulipigwa saa Kumi kamili katika uwanja wa Vwawa wilaya ya Mbozi. Katika mchezo huo Timu ya Panone Fc ilihitaji Ushindi ili iweze kufuzu mashindano Huku nayo timu ya Njombe Mji ya Mkoa wa Njombe ikiwa inachuana na Timu ya AFC ya Arusha katika uwanja wa Mbeya Mjini huku Njombe wakiwa wanahitaji Ushindi na kuiombea Panone Fc ipoteze mchezo ili iweze Kushinda.
Katika Mchezo wa Jana Hali ilikua tofauti mnamo wa Dakika ya Tatu Mchezaji wa Panone Fc Ramadhan Hasan Aliweza kuiandikia Goli la Kwanza Timu yake na kuamsha Mashambulizi na Hari mpaka Dakika ya Sita ya Kipindi cha kwanza ndipo Ayoub Ruben alipoifungia Goli la Pili Timu ya Panone Fc na kuyazima matumaini ya Timu ya Small Town ya Ruvuma. Mpaka Mpra kuisha Panone Fc ilipata ushindi wa Goli mbili kwa bila dhidi ya Small Town ya Ruvuma huku Timu ya Njombe Mji na AFC ikitoka Sare ya Goi moja kwa moja na Matokeo hayo yakazima ndoto za Timu ya Njombe mji huku Nyota ya Panone Fc iking'ara.
Tulipata Fursa ya kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Panone and Co. Ltd Ndugu Patrick Ngiloi Kupitia Kampuni yake ndio wanaoiwezesha timu hiyo aliweza kuzungumzia mafanikio ya timu hiyo huku akisema mafanikio hayo ni ya Mkoa wa kilimanjaro yeye kama mdau kupitia kampuni yake ameweza kuwaweka vijana pamoja na kujiajiri katika michezo na kuwaepusha na Uvutaji wa Dawa za kulevya na hata uhalifu na kujikita katika michezo na Heshima hii si ya Kampuni ya Panone Pekee ni heshima kwa Mkoa Mzima wa Kilimanjaro na Akawataka wakazi wa mkoa wa Kilimanjaro waiunge mkono Timu hiyo iweze kufika mbali.
Wachezaji wa Panone wakishangilia ushindi
Mashabiki wa Mabingwa wapya wa RCL, Panone FC wakishangalia ushindi
Ni furaha tupu...
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :