BRAZIL BILA NEYMAR WATAWEZA KUVUNJA UKUTA WA UJERUMANI LEO?
Posted in
Michezo
No comments
Tuesday, July 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Hatua za nusu fainali za michuano ya Kombe la Dunia huacha historia isiyofutika katika ulimwengu wa soka.
Wakati mwingine ile ari, nguvu na kasi inayotumika kutaka kufika hatua
ya mwisho hutoa ushindani ambao wakati mwingine huzidi hata fainali
yenyewe.
Ni timu nne zinazotaka kujihakikishia zinafika fainali ili kumtwaa
mwali, na kwa kuanzia Jumanne hii majira ya saa 5 usiku, kwa saa za Afrika mashariki, itawashuhudia wenyeji Brazil
waliojeruhiwa wakishuka dimbani kuchuana na Ujerumani.
Vijana wa Luiz Felipe Scolari wanashuka dimbani wakiwa hawana nyota
wao wa ushambuliaji, Neymar Jr. aliyeumizwa uti wa mgongo katika mechi ya
robo fainali dhidi ya Colombia na pia hawatakuwa na nahodha wao, Thiago
Silva ambaye anatumikia adhabu ya kupata kadi mbili za njano.
Neymar alijikuta akipoteza ndoto ya kuiongoza brazil kutwaa Ubingwa wao wa Sita huku pia ndoto zake za kutwa kiatu cha dhahabu zikizimwa baada ya kuumizwa vibaya katika maeneo ya mgongoni na Beki wa Colombia, twaa Ubingwa kumbana Kocha Scolari anajipa moyo na kuwatuliza washabiki wao, akisema
kwamba wanaweza kucheza vyema hata bila ya kuwapo Neymar uwanjani, huku
Silva akiwataka wenzake wahakikishe wanashinda ili iwe zawadi kwa Neymar
(22).
Kinda huyo ndiye amefunga mabao manne kati ya manane waliyo nayo
Brazil hadi sasa lakini Scolari anasema kikosi chake kina ari kubwa,
kikiwa tayari kuwavaa Wajerumani. Mshambuliaji wao mzuri, Fred,
alionekana kutokuwa vyema sana kwenye mechi zilizopita.
“Neymar ameshatoa mchango wake, sasa ni juu yetu kutoa wa kwetu.
Tumeshapokea yaliyotokea na sasa tunajielekeza kwenye mambo mengine,”
anasema Scolari akiwa hataki kuzama kwenye suala moja la kumkosa Neymar
tofauti na wanahabari wanavyopenda.
Neymar alitenguliwa pingili ya uti wa mgongo na mchezaji wa Colombia,
Juan Zuniga aliyemgonga kwa goti kutoka nyuma na kumpa maumivu makali
kiasi cha kulia machozi kwa sauti kubwa uwanjani hadi akiwa hospitalini.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Low alisema kwamba anadhani Wabrazili ni
wazuri bado na kwamba wanaweza kuwasababishia majanga, ila
akamhadharisha mwamuzi wa mechi hii, Marco Antonio Rodriguez kuwa makini
na kuchukua hatua dhidi ya kila rafu lakini pasipo kuonea wala
kupendelea upande wowote.
Mjerumani huyo anasema kwamba mechi baina ya Brazil na Colombia
ilihusisha kutunishiana misuli na rafu nyingi sana na si dhidi ya Neymar
pekee, akisema kwamba hajapata kuona soka ya aina hiyo Ulaya, akamtaka
mwamuzi awalinde wachezaji muda wote wa mchezo.
Mechi hii inapigwa katika dimba la Estadio Mineirao, jijini Belo
Horizonte, uwanja unaokalisha watazamaji zaidi ya 62,000, ambapo watu
waliowasili kwenye uwanja wa ndege jijini humo Jumatatu hii walipokewa
kwa bendera na mabango ya Brazil, wakiwa na hamu ya kununua tiketi kwa
ajili ya mechi hii kubwa.
Brazil wamekutana na Ujerumani katika Kombe la Dunia mara moja tu,
mwaka 2002 katika fainali nchini Japan, ambapo Scolari aliwaongoza
vijana wakashinda 2-0 na kutwaa kombe hilo.
Ujerumani wanacheza nusu fainali ya nne mfululizo katika mashindano
haya tangu wakati huo, Low akisema vijana wake watakuwa kana kwamba
wanakabiliana na nchi nzima ya Brazil, kwani watakuwa wanaungwa mkono na
watu milioni 200.
Rekodi ya timu hizi ikoje?
Katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002, zilizofanyifanyika Korea Kusini na Japan, Brazil iliifunga Ujerumani 2-0, kupitia mshambuliaji wake hatari, Ronaldo de Lima.hizi hapa ni baadhi ya matokeo kati ya mataifa haya mawili, walipokutana katika michuano mbali mbali tano ya hivi karibuni, ukiacha hili la 2002.
2011 mchezo wa kirafiki: Germany 3-2 Brazil
2005 Confederations Cup: Germany 2-3 Brazil
2004 mchezo wa kirafiki: Germany 1-1 Brazil
1999 Confederations Cup: Brazil 4-0 Germany
1998 mchezo wa kirafiki: Germany 1-2 Brazil
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :