UHOLANZI DHIDI YA ARGENTINA NI MECHI YA KUONESHANA UMWAMBA; NANI ATAINGIA FAINALI?
Posted in
Michezo
No comments
Tuesday, July 8, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Argentina na Uholanzi wanakutana kesho katika mchezo wa nusu fainali ya Pili ya kombe la dunia mwaka 2014 itakayopigwa katika uwanja wa Arena Corinthians, mjini Sao Paulo, huku swali kubwa likiwa ni nani ataibuka mbabe katika mpambano huu ambao wengi wanautafsiri kama mechi ya kuoneshana umwamba?
Hata hivyo, haimaanishi kwamba mchezo kati ya timu hizi mbili haitakuwa ya kuvutia ukizingatia ukweli kwamba Argentina na uholanzi wote wana kiu ya kutwaa Kombe hili katika ardhi ya bingwa mara tano, Brazil.
Uholanzi wanaonekana Bora
Ubora wa Uholanzi ulianza kudhihirika baada ya kuwakandamiza Bingwa watetezi, Uhispania goli 5-1, kabla ya kutoka sare ya 0-0 na timu ngumu ya Costa Rica, wakiinyuka Australia 3-0, Chile wakila 2-0 na magoli ya mwisho mwisho waliopata katika hatua ya 16 bora dhidi ya Mexico na kubadili mchezo yanatosha kukuonesha kuwa Vijana hawa wameamua mwaka huu.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :