MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA WANAWAKE WATANZANIA WAJASIRIAMALI WA DMV JIJINI WASHINGTON
Posted in
Matukio
No comments
Monday, August 4, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu
Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake
wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies
Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani tarehe 3.8.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Help for Underserved Communities (HUC) ya
nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma
mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia
maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia
visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
Baada
ya kutembelea maonesho ya wanawake wajasiriamali Mama Salma Kikwete
akifuatana na Afisa Tawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama
Lily Munanka kwenda kuweka saini kwenye kitabu cha wageni.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha wageni.
Aliyesimama kushoto ni Bibi Lily Munanka, Afisa wa Ubalozi wa Tanzania
nchini Marekani.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa wana kikundi wa TANO
Ladies. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti Asha Hariz, akifuatiwa na Asha
Nyang’anyi, Isca Kauga, Juster Mutakyawa na Tumaini Kaisi aliyeshika
kipaza sauti.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kikundi cha TANO
Ladies cha nchini Marekani. Anayekabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya
wanakikundi wenzake Ndugu Juster Mutakyawa.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania
wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya
ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.
Baadhi
ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini
Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiagana na baadhi ya wanawake mwishoni mwa
mazungumzo yake na wanawake hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya
ubalozi wa Tanzania nchini Marekani huko Washington tarehe 3.8.2014.
Mke wa Rais akipiga picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
Balozi
wa Tanzania nchni Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula akimuaga Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kutembelea ofisi za ubalozi huo
na kuongea na wanawake wa Tanzania wanaoishi nchini Marekani. PICHA NA
JOHN LUKUWI.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :