DIEGO COSTA, CESC FABREGAS NA JOSE MOURINHO USO KWA USO TUZO YA MWANASOKA BORA WA MWEZI ENGLAND

Posted in
No comments
Thursday, September 11, 2014 By danielmjema.blogspot.com

WADHAMINI wa Ligi Kuu England wametangaza Listi ya Wagombea wa Tuzo za Mwezi za Meneja Bora na Mchezaji Bora na miongoni mwao ni Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, huku Wachezaji wake Diego Costa na Cesc Fabregas wakiwemo.
Kwa upande wa Mameneja yupo pia yule wa Swansea City Garry Monk ambae ameiongoza Timu yake kushinda Mechi zao zote 3 za kwanza za Ligi na pia yuko Meneja wa Stoke City Mark Hughes ambae Timu yake iliwafunga Mabingwa Manchester City katika Mechi iliyopita huko Etihad.
Pia yupo Paul Lambert wa Aston Villa ambae Timu yake imeshinda Mechi mbili na Sare moja. Kwa upande wa Wachezaji yuko Straika wa Chelsea Diego Costa ambae ameifungia Timu yake Bao katika kila Mechi ya Ligi waliyocheza na pia yumo Kiungo wa Timu hiyo Cesc Fabregas ambae amekuwa aking’ara katika Mechi zote.

Wengine ni Nathan Dyer wa Swansea ambae amepiga Bao 3 na pia yuko Mchezaji mwenzake wa Timu hiyo Gylfi Sigurdsson. Wa mwisho kwenye Listi ya Wagombea kwa Wachezaji ni Mchezaji wa Aston Villa Andreas Weimann ambae ameifungia Timu yake Mabao ya ushindi dhidi ya Stoke na Hull City.
BPL-LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 13
1445 Arsenal v Man City
1700 Chelsea v Swansea
1700 Crystal Palace v Burnley
1700 Southampton v Newcastle
1700 Stoke v Leicester
1700 Sunderland v Tottenham
1700 West Brom v Everton
1930 Liverpool v Aston Villa
Jumapili Septemba 14
1800 Man United v QPR
Jumatatu Septemba 15
2200 Hull v West Ham
***KWA RATIBA KAMILI YA MSIMU WOTE BOFYA: http://www.sokaintanzania.com/ligi-kuu-england

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .