MKUTANO WA 24 WA MWAKA WA WANACHAMA NA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF WAANZA RASMI LEO JIJINI ARUSHA

No comments
Wednesday, September 10, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 24 wa Mwaka wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF,Naibu Waziri wa Fedha, Mh. Mwigulu Nchemba akitoa hotuba yake wakati akifungua mkutano huo unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC,jijini Arusha kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo Septemba 10 mpaka Septemba 12,2014.
Katika hotuba yake hiyo,Mh. Nchemba wameutaka Mfuko wa PPF kuhakikisha wanapanua wigo kwa kuongeza wanachama wengi kutoka kwenye setka binafsi hasa wananchi wa kipato cha chini ikiwemo wajasiriamali.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa Mkutano wa Wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaoendelea Kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC
Naibu Waziri wa Fedha, Mh Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati wa Mkutano wa wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaoendelea katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC, Jijini Arusha.
Mgeni Rasmi katika Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF ambae pia ni Naibu Waziri wa Fedha Mh Mwigulu Nchemba akiwa katika Picha ya Pamoja na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii mara baada ya Kufungua Mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha
Naibu Waziri wa Fedha, Mh Mwigulu Nchemba akimpongeza Meneja Masoko na Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Lulu Mengere wakati wa mkutano wa 24 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC, Jijini Arusha

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .