WAFANYAKAZI WA BENKI YA NBC WAJIMWAGIA MAJI BARIDI KUCHANGISHA FEDHA KUPAMBANA NA UGONJWA WA FISTULA

Posted in
No comments
Monday, September 15, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Mkuu wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe (kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto) akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati) naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa fistula nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Binafsi na biashara ndogondogo na za kati, Isidori Msaki (katikati) akijitahidi kujizuia wakati wafanyakazi wenzake wakimmwagia ndoo za maji baridi katika hafla hiyo.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .