CBA YATANUA KWENYE M-PAWA

Posted in
No comments
Wednesday, October 8, 2014 By danielmjema.blogspot.com

DSC_0055
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo akizungumza wakati kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wao kwa kuichagua CBA pamoja na kuwapongeza wafanyakazi wa benki yake kwa kutoa huduma nzuri kwa wateja wao katika mkutano na wanahabari uliofanyika kwenye tawi la CBA Kariakoo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru na Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa (aliyesimama kushoto).(Picha na Zainul Mzige).

DSC_0001
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo (aliyekaa kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wa benki ya CBA ambapo watatumia wiki hii kusikiliza nini wateja wao wanataka. Waliosimama kutoka kulia ni Meneja wa tawi la CBA Kariakoo, Vicky Munishi, Boniface Kiwia kutoka makao makuu ya CBA, Tanzania, Rehema Mashayo kutoka makao makuu wa benki ya CBA Tanzania. na kushoto ni Afisa viwango na ubora wa huduma CBA Tanzania, Anicetius Buberwa.

DSC_0080
Meneja anayeshughulikia wateja wa CBA Tanzania, Rehema Ngusaru akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wakitangaza rasmi kuzindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja watakayoitumia kusikiliza changamoto wanazokutana nazo wateja wao.
Alisema benki hiyo ambayo ina matawi matano Dar es salaam na mengine yakitawanyika katika miji ya Mtwara, Mbeya,Arusha, Tunduma imejitanua katika kutoa huduma kwa kutumia teknolojia hasa kwa kuwa na huduma za kibenki kwa njia ya mtandao.
Alisema kupitia njia ya mtandao wateja wao wanaweza kupata mikopo na hata kulipa huduma mbalimbali.
Aliwashukuru wateja na wafanyakazi kwa kuwezesha ndoto za wengi kutimia kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo na kuwataka waendelee kutumia CBA katika kuchupa mbele kimaendeleo.
Baadhi ya wateja waliohojiwa katika uzinduzi huo walikiri kufurahishwa na huduma za benki hiyo hasa kutokana na kutokuwa na foleni na kujali wateja wao.
Charles Mlawa alisema kwamba wamefurahishwa sana na uwapo wa tawi la CBA Kariakoo kwani limefanya waweze kuwa na uhakika na utumaji wa fedha kwa wadau wao ili kupata bidhaa zinazotakiwa.
DSC_0091
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA), Julius Mcharo akitoa huduma kwa mkazi wa jijini Dar Bw. Ali Sareva aliyefika kwenye tawi la benki ya CBA lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua akaunti ya kampuni yake wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa ulimwengu mzima ambapo benki ya CBA wataadhimishi wiki hiyo kwa kusikiliza nini wateja wanachokitaka na kuwa nao karibu zaidi kuboresha huduma zao.

DSC_0097
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo akimshukuru mkazi wa jijini Dar Bw. Ali Sareva kwa kuiamini na kuichagua benki ya CBA inayowajali wateja wake.
DSC_0108
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Commercial Bank of Africa (CBA) Tanzania, Julius Mcharo akimhudumia mmoja wateja wakubwa wa benki hiyo mfanyabiashara maarufu Kariakoo Bw. Charles Mlawa kwenye tawi la benki hiyo lililopo Mtaa wa Narung'ombe Kariakoo jijini Dar es Salaam katika kuadhomisha wiki ya huduma kwa wateja.
DSC_0121
Mkuu wa biashara na uendeshaji wa kampuni ya vifaa vya umeme ya Tropical ambaye pia ni mteja wa benki ya CBA tawi la Kariakoo, Bw. Charles Mlawa, akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema wamepata faida kubwa sana kwa benki ya CBA kuwepo Kariakoo akiwa yeye kama mteja wa siku nyingi wa benki hiyo ambapo pia ameipongeza benki hiyo kwa huduma bora na yenye uhakika ya gharama nafuu kabisa ambayo ni sawa na bure ya TT katika utumaji wa fedha. Katikati ni mteja mwingine wa benki ya CBA Tanzania, Bw. John Nenuta.
DSC_0134
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo (waliosimama wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wateja wa benki ya CBA tawi la Kariakoo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo kutoka makao makuu ya CBA Tanzania na wafanyakazi wa tawi la Kariakoo.
DSC_0137
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo akiagana na mmoja wa wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.
DSC_0141
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) Tanzania, Julius Mcharo katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .