TAMASHA LA SANAA NA UTAMADUNI LA KIMATAIFA JAMBO FESTIVAL KUFANYIKA JIJINI ARUSHA.

Posted in
No comments
Friday, October 3, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Wasanii wa muziki wa asili wakitoa burudani katika tamasha la Jambo festival.
Mwenyekitiwa Tamasha la sanaa na utamaduni Arusha  maarufu kama JamboFerstival   Augustine Michael Namfua

Jiji la Arusha litatikiswa na tamasha la sanaa  na utamaduni la
kimataifa maarufu kama Jambo festival litakalojumuisha ngoma za asili,mavazi ya asili, muziki wa asili, mavazi na vyakula, tamasha hilo litatikisa viunga vya jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha utalii.

Takribani watu 3000 kutoka sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi 
wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo ambalo hutoa burudani isiyo kifani 
na lenye kila aina ya ubunifu .

Wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki Kenya, Rwanda, Burundi, Nchi za 
Ulaya, Marekani na Asia wanatarajia kuhudhuria huku wenyeji wao wakiwa 
ni wakazi wa Arusha.

Mwenyekiti wa Tamasha  la Jambo Festival, Augustine Michael Namfua 
anaeleza kuwa tamasha hilo limekua likifanyika miaka 2 mfulululizo na 
kwa sasa  linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sanaa na utamaduni.

Augustine anaeleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha hilo 
lengo ni kuonyesha kazi za sanaa hususani tamaduni.

Tamasha hili limekua likiwaunganisha kwa pamoja wapenzi wa sanaa na 
utamaduni wa Watu wa Arusha,Tanzania  na Afrika  kwa ujumla hasa 
ukizingatia kuwa Arusha ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki 
na ni mji wa utalii.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .