WANAWAKE WA INDIA WATEMBELEA VIKUNDI VYA WANAWAKE WAJASIRIAMALI MKURANGA
Posted in
Matukio
No comments
Monday, November 17, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiajiri wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kuranga wakati walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo wilayani hapo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila na mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akizungumza na Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete. Kushoto ni mlezi wa Kikundi cha Kiwalani Women Group ambaye pia ni mke wa mbunge wa Mkuranga, Naima Malima.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Mercy Sila akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Wanachama wa Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), Labhu Thakkar walipotembelea vikundi vya wajasiriamali vilivyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, pamoja na kutembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete.
Mkutano ukiendelea kabla ya wageni kutoka Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) kutembelea Zahanati ya Kijiji cha Msufini Kidete iliyopo Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Wachama wa Ushirika Sewa wakiwa katika mkutano na uongozi wa Kijiji cha Msufini Kidete Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Mtendaji wa Kijiji cha Msufini Kidete, Seleman Kayombo akitoa taarifa fupi za utendaji wa kijiji hicho kwa wageni waliofika kutoka Ushirika wa Wanawake waliojiajiri wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea Zahanati ya Kijiji hicho.
Mkurugenzi wa Mradi wa Sankalit Sewa, Shree Kant Kumar akizungumza wanakijiji wa Msufini Kidete wakati Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA) walipotembelea miradi ya maendeleo ikiwemo afya.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Msufini Kidete wakiwasikiliza wageni waliofika kijijini hapo kutoka katika Ushirika wa Wanawake waliojiairi wenyewe kutoka India (SEWA), walipotembelea Zahanati ya kijiji cha Msufini Kidete Mkuranga.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :