ESCROW: IKULU YAZIIDI KUMLEA MUHONGO

Posted in
No comments
Saturday, December 27, 2014 By danielmjema.blogspot.com

Waziri wa Nishati na Madini akiulizia utekelezaji wa umeme katika kijiji cha Kamgendi katika siku yake ya kwanza ya siku 6 za ziara katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara

 
Licha ya watu mbalimbali kutaka Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusiana na sakata la fedha za escrow, Ikulu imesema suala hilo litatolewa uamuzi wakati wowote baada ya mapumziko ya sikukuu.

Hivi sasa Rais yupo katika mapumziko ya Sikukuu za Krismasi inayosherehekewa Desemba 25 kila mwaka na Mwaka Mpya itakayofanyika Januari Mosi.

Akizungumza na wazee wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka huu, Rais Kikwete alisema amemweka kiporo waziri huyo hadi atakapopata ufafanuzi wa mambo kadhaa na kwamba atakapojilidhisha ataujulisha umma.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete bado hajakamilisha kulishughulikia suala hilo na kwamba litakapokuwa tayari wananchi watajulishwa hatua alizozichukua.
“Unakumbuka Rais alichosema? Bado analifanyia kazi, atakapomaliza tu mtajulishwa, sasa hivi ni kipindi cha sikukuu,” alisema Sefue.

Profesa Muhongo
Hata hivyo, Profesa Muhongo alipotakiwa kuzungumzia shinikizo linalotolewa la kutaka ajiuzulu kabla ya Rais Kikwete kutoa uamuzi wake, aliliambia gazeti hili jana kwa simu kuwa; “Mimi sasa sitaki kuzungumza na waandishi, mambo yangu yote wapo watu ambao wanaweza kuyazungumzia.”

Hata hivyo, katika hotuba yake, Rais Kikwete aliagiza kuchukuliwa hatua kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma kuhusu ushiriki wake kwenye kashfa hiyo.

Siku iliyofuata, Sefue alimweka ‘kando’ Maswi na kumteua Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava kukaimu nafasi hiyo hadi uchunguzi utakapokamilika.

Kutokana na kuchelewa kutekelezwa kwa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi hao kuwajibishwa, Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umeahidi kuwasilisha hoja bungeni ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu na kufanya maandamano nchi nzima. 

Mpaka sasa viongozi watatu wameshakumbwa na dhoruba inayotokana na sakata la escrow baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema, kung’olewa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na kuwekwa kando kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Maswi.

Wapinzani Zanzibar wakoleza moto 
Chanzo:Mwananchi

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .