TAMKO LA MECKI DHIDI YA MAHUSIANO YASIYORIDHISHA KATI YA WAANDISHI WA MKOA WA KILIMANJARO NA RPC, ACP GEOFREY KAMWELA

No comments
Tuesday, December 23, 2014 By danielmjema.blogspot.com


Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Kilimanjaro (MECKI), Rodrick Makundi (Aliyesimama) akatika moja ya mafunzo. (Picha na Maktaba Yetu).

Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro [MECKI] imepokea kwa masikitiko malalamiko ya baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro kuhusu mahusiano yasiyoridhisha ya kikazi baina yao na kamanda Kamwela.

Baada ya kupokea malalamiko hayo, viongozi wa klabu walijaribu kumtumia mkuu wa mkoa wa KILIMANJARO, Leonidas Gama kurekebisha hali hiyo, lakini bado juhudi hizo hazijazaa matunda mpaka sasa.

Kufuatia mahusiano hayo kuendelea kuzorota siku hadi siku, na klabu ikiendelea kusubiri hatua za Mkuu wa mkoa, imelifikisha suala hilo ngazi za juu za Jeshi la Polisi, kwa lengo la kutafuta njia itakayosaidia kuimarisha uhusiano wa kikazi kati ya Jeshi la Polisi Kilimanjaro na waandishi.

Kimsingi Klabu wala waandishi hawana tatizo la Kamanda Kamwela, na Klabu haijatumia nafasi hiyo kuleta matatizo na viongozi wake wajuu, inachokifanya ni kulifikisha jambo hili ngazi za juu kwa mtazamo wa kutafuta utaratibu mzuri wa upatikanaji wa habari ndani ya Jeshi hilo Kilimanjaro, na kuua tatizo la kimfumo unaoleta ukakasi kwenye upatikanaji wa habari zinazohitaji kuthibitishwa na Jeshi hilo.

Bado Jeshi la Polisi lina nafasi kubwa ya kusaidia kupatikana kwa habari kirahisi ili kuwahabarisha na kuwaelimisha watanzania, na nafasi hii inaboreshwa zaidi na uhusiano mzuri utakaokuwepo baina ya pande hizi mbili.

Pamoja na yote Klabu inawaomba waandishi wote Kilimanjaro kuendelea kuwa wavumilivu kwa sasa na kuendelea kusimamia maadili ya uandishi wa habari, kwa kuwa mazungumzo ya Uongozi wa Klabu na makao makuu ya Jeshi la Polisi na mkuu wa mkoa pia yanaenda vizuri tukiamini ufumbuzi utapatikana ndani ya muda mfupi ujao.

Rodrick Makundi
Mwenyekiti, MECKI, December 20, 2014

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .