MBUNGE WA CHALINZE, RIDHIWANI KIKWETE AANZA ZIARA YA KIKAZI KATIKA VIJIJI 40 JIMBONI KWAKE

Posted in
No comments
Saturday, January 3, 2015 By danielmjema.blogspot.com

Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akikagua vyumba vya madarasa vya Shule ya Msingi Kibindu, wilayani Bagamoyo, Pwani vilivyobmoka na kuezuliwa paa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni. Ridhiwani yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea vijiji 40 jimboni humo. Pia Ridhiwani alishauri shule hiyo yenye majengo yaliyojengwa tangu 1952 ifungwe ili kuepusha maafa zaidi hadi itakapojengwa upya.
 Ridhiwani akinunua ndizi na kuzigawa kwa watoto katika Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa ziara yake jimboni Chalinze jana.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu, ambapo aliwapongeza wananchi kuchagua viongozi wa Serikali ya Vijijini kutoka CCM.
Watoto wakiruka mtaro kumuwahi Ridhiwani Kikwete alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika Kata ya Kibindu
Ridhiwani akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kijiji cha Kwa Msanja wakati wa uzinduzi wa Kisima cha Maji kilichojengwa kwa fedha za mfuko wa jimbo kwa gharama ya sh. mil. 13.
 


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .