KNCU YASHUSHA MTAMBO MPYA WA KUKOBOA KAHAWA KUTOKA BRAZIL.

Posted in
No comments
Tuesday, February 17, 2015 By danielmjema.blogspot.com

Na Athumani Issa wa Kijiwe chetu Blog, Moshi

KATIKA harakati za kuboresha uzalishaji wa zao la Kahawa, Chama cha Ushirika cha Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kilimanjaro (KNCU), kimenunua mitambo mipya ya kukoboa Kahawa, yenye thamani ya dola laki 9.48 za kimarekani, iliyoagizwa kutoka Brazil.

Mwandishi wa mtandao wa KIJIWE CHETU BLOG alifika katika viwanja vya Kiwanda cha kukoboa Kahawa (TCCCO), kinachomilikiwa na KNCU na kushuhudia magari matano, aina ya Scania, yakipakua mitambo ya kisasa ambayo ni ya kwanza katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.

Uagizwaji wa mitambo hiyo ni moja ya maazimio ya mkutano mkuu wa KNCU kilichofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo wajumbe waliazimia kuwa  juhudi za makusudi zifanyike kunusuru kiwanda hicho.

Akizungumza na Mtandao huu, Meneja wa TCCCO, Endrew Kleruu, alisema mitambo hiyo itasaidia kupunguza upotevu wa kahawa,ikiwa ni pamoja na kuongeza ubora wa uzalishaji unaoendana na viwango vya ubora katika soko la Kimataifa.

Alisema mitambo hiyo yenye uwezo wa kuzalisha tani sita kwa saa moja itasaidia kuwapunguzia wakulima gharama za uzalishaji kutokana na uwezo wake wa kutumia umeme mdogo (30-35 KV) tofauti na mitambo wa zamani ambayo ilikuwa inazalisha tani nne tu kwa saa, ikitumia zaidi ya  100KV ya umeme.

Kwa upande wake meneja wa usambazaji vifaa wa kampuni ya Brazafric Enterprizes Ltd, Salim Mghweno, alisema kuwa ufungaji wa mitambo hiyo itatumia miezi miwili ambapo matarajio ni hadi kufikia msimu wa uzalishaji wa Kahawa mitambo huu umeshakamilika.


Mtambo mpya wa kisasa wa kukobolea Kahawa ulionunuliwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa zao la Kahawa mkoani Kilimanjaro kwa gaharama za dola laki 9.48 ukishushwa katika kiwanda.
Mota ya kuzungusha mashine wakati wa ukoboaji ikishushwa ikiwa ni sehemu ya mtambo mpya wa kukobolea Kahawa utakaofungwa katika kiwanda cha Cofee Curing.
Sehemu ya vifaa kwa ajili ya mtambo mpya wa kisasa wa kukobolea Kahawa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .